Header Ads Widget

MWWNYEKITI LNG MHANDISI SANGWENI AVUTIWA NA UTENDAJI KAZI KIWANDA CHA GESI MADIMBA

 


Na Matukio Daima App Mtwara 

Mwenyekiti wa Timu ya majadiliano ya mradi wa LNG Mhandisi Charles  Sangweni  amefurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda cha kuchakata gesi cha madimba mtwara kutokana na watalaamu wa kiwanda hicho kuwa watanzania pekee. 


Akizungumza alipotembelea kiwanda hicho alisema  kitendo cha watumishi hao kuwa ni watanzania inaonyesha wazi kuwa tumepiga hatua kubwa katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za nchi yetu. 


Aidha amesema kuwa ameweza kutembelea kiwanda cha kuzalisha gesi asilia Mnazi bay na kiwanda cha kuchakata gesi asilia Madimba ikiwa ni sehemu ya kujifunza wakati wa maandalizi ya mradi wa LNG utakaojengwa mkoani Lindi kwa gharama ya USD bilioni 30. 


"Nimefurahishwa sana na kiwanda hiki hii inaonyesha wazi kuwa serikali ilijiandaa na ilifanikiwa kwa hili tunaweza kufanya maandalizi ya LNG na tukafanikiwa ni jambo kubwa lakujivunia kuona watalaamu wazawa wakiendesha mitambo na kutuzalishia gesi asilia Shirika letu la Petrol Tanzania (TPDC) linafanyakazi nzuri kwakuwatumia wazazwa kuendeleza rasilimali zetu" alisema Sangweni


"Huu mradi ni mkubwa hebu fikiria makisio tu ni USD Bilioni 30 unaweza kuuona ukubwa wake hii inatosha kuwaamsha watanzania ili waweze kujiandaa kupokea fursa hizo adhimu"


Mradi huu utachukua miaka 4-5 kukamilika ajira mbalimbali zaidi ya 5000 zitakuwepo za moja kwa moja lakini kuna zile ambazo sio za moja kwa moja zitakuwa kwenye  3000-6000 ili uzipate lazima uonyeshe utayari na ujiandae kuzipokea"  


Kwa upande wake mjumbe wa timu hiyo Prof Sifuni Mchome alisema kuwa uwepo wa gesi asilia uongeze hali na hamasa kwa watanzania kufanyakazi ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zitokanazo na rasilimali hiyo.


"Katika ziara hii tumekuja kujifunza na kuzungumza na wenzetu ili kuona na kujifunza ili kufahamu manufaa gani tutapata na tungependa hii gesi asilia ilite faida gani kwetu? 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI