Header Ads Widget

MKURUGENZI TEMDO ADAI KUBAINI TEKNOLOJIA HII

 



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania TEMDO,Injinia Fredrick Kahimba akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uwepo wa vifaa mbalimbali vya hospitali vinavyotengenezwa na Taasisi hiyo

Na Pamela Mollel,Matukio Daima APP Arusha 

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO)Injinia Frederick Kahimba amesema wamebuni Teknolojia mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali zitakazo wezesha watanzania  kuagiza vifaa hivyo hapa nchini 


Aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea Taasisi hiyo kwa lengo la kujifunza na kuandika habari za Sayansi na Teknolojia iliyofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania(COSTECH)


Alisema kuwa Teknolojia hizo ni pamoja na Majokofu ya kuhifadhi miili,Vitanda vya kujifungulia kinamama na viteketeza taka katika hospitali



"Taasisi hii imekuwa ikibuni vifaa mbalimbali vya hospitali na asilimia 80 ya vifaa hivi vinaagizwa nje ya nchi,ni fursa kwa watanzania kuchangamkia hili kwa kuagiza hapa nchini "alisema  Kahimba


Injinia  Kahimba alisema kuwa uwepo wa vifaa hivyo hapa nchini  itasaidia watanzania kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo 

Aliongeza kuwa wanashukuru COSTECH kwa kuwawezesha fedha za kufanya utafiti kiasi cha shilingi milioni 128na kati ya hizo milioni 65 walitumia kwaajili ya mtambo wa kusafishia mafuta ya alizeti



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI