Header Ads Widget

MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE ATOA ONYO KALI

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick akizungumza na Walimu wakuu Na Maofisa Watendaji wa Kata,Vijiji na Mitaa Juu ya Manunuzi ya Umma


Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima APP NJOMBE

BAADHI ya Wakuu wa Shule,Wasimamizi wakuu wa Vituo Vya Afya na Zahanati na Maofisa Watendaji Wameonywa Vikali Juu ya Tabia ya Kujihusisha na Wizi wa Fedha za Miradi ya Afya na Elimu Inayotekelezwa Katika Maeneo Yao Kwa Kufanya Makubaliano maovu na Mafundi Pamoja na Wauzaji wa Vifaa Vya Ujenzi.

Mkurugenzi  mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji ya Njombe Kuruthum Sadick Ametoa Onyo Hilo Wakati Akifungua Mafunzo ya Masuala ya Manunuzi Kwa Walimu Wakuu,Waganga wakuu wa Vituo Vya Afya na Zahanati Pamoja na Maofisa Watendaji wa Kata,Vijiji na Mitaa Ili Waende Kutekeleza Ujenzi wa Miradi ya Serikali kwa Weledi na Uadilifu mkubwa.

Amesema Kwenye Makubaliano ya kuweka Cha Juu na Mafundi Ujenzi ndani yake wapo Maofisa Usalama Hivyo Walimu Hao Wanapaswa kuwa makini na Kuacha tamaa za fedha zitakazowaingiza matatani.

Awali Afisa Elimu Msingi Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Zegeli Shengelo Amesema Hatua Hii Inakuja Kutokana na Kuwapo Kwa Madiliko ya Sheria na Miongozo ya Manunuzi Katika Miradi ya Serikali Ambapo Walimu Wakuu Ndio Wasimamizi Wakuu wa Miradi Hiyo Kwenye Shule Zao.

Baadhi ya Walimu Wakuuu Hao Akiwemo Lwimo Samizi na Emmanuel Haule Wanakiri Kuwa Miradi Hiyo ni Muhimu Sana Katika Maendeleo ya Shule Zao Lakini Imekuwa Mwiba Kwao Katika  Utekelezaji kwani imekuwa ikiwasababishia kupoteza muda mwingi kwa kushindwa kuhudhuria vipindi darasani,Gharama kubwa za ufuatiliaji ambazo hazipo kwenye bajeti ya mradi na kuwafanya kuanza kutumia fedha yao binafsi.

Akitolea Ufafanuzi wa Malalamiko ya Walimu Wakuu Hao Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mwangaza Kusenge  Amekiri kuwapo kwa changamoto hizo na kwamba kwa miradi inayotoka Serikali kuu imekuwa haina fedha za ufuatiliaji lakini kwa miradi inayotokana na mapato ya ndani ataliwasilisha kwa Mkurugenzi ili kuona namna ya kushughulikia.

Matumizi Mabaya ya Fedha za Serikali Imekuwa Ikiwapeleka Jela Watumishi Wengi wa Serikali Pamoja na Watu Binafsi Kutokana na Uroho wa Kutaka Kupata Mali Kwa Njia Zisizo Halali.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI