Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi amempongeza Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe kwa hatua za haraka alizochukua kunusuru maisha ya askari waliojeruhiwa katika ajali ya gari iliyouwa watu wanne wakiwemo askari wawili wa Jeshi hilo.
Akizungumza katika shughuli ya kuaga miili ya askari hao iliyofanyika katika uwanja wa Polisi Mabatini, Ng'anzi pia amewataka wafiwa kuwa na subira katika kipindi kigumu wanachopitia.
Amesema mbali na kuwa waadilifu, askari hao pia walijitoa kutumikia jeshi hilo na taifa huku akitoa wito kwa askari wengine kuiga matendo mema ya askari hao.
Akisoma wasifu wa askari hao, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Ilemela, Shamira Mkomwa amesema makachero hao wameacha wajane na watoto wawili kila mmoja.
Naye kaka wa marehemu (Mussa), Mwita Muhamba amesema kifo cha ndugu yake kiliishtua familia huku akiahidi kuendeleza matendo mema ya ndugu yao.
Mwisho.
0 Comments