Na Mwandishi Wetu,
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa na ujumbe wa Tanzania, wameshiriki mkutano wa Mashauriano ya Mawaziri wa Ardhi wa Nchi za Afrika, wenye agenda ya Miji mipya, katika makao makuu ya UN-HABITAT.
Mkutano huo ulioandaliwa na UN-HABITAT, uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-HABITAT, Bi. Maimuna Mohamed Sharif ambaye alipongeza juhudi zinazofikiwa katika kuendeleza miji na makazi katika Bara la Afrika.
"Nimefurahi kuwa miongoni mwa Mawaziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miji wa Afrika leo, Nimetiwa moyo na maono yao juu ya ukuaji endelevu wa miji na makazi Barani Afrika." Alisema Bi. Maimuna Sharif
Na kuongeza kuwa:
"Ahadi ya UNHABITAT ni kuhakikisha inaendelea kusaidia nchi wanachama na sekta binafsi katika Umoja wa Afrika (UA),
Ikiwa ni pamoja na kuchukua jukumu muhimu katika kuinua umuhimu wa ukuaji wa miji na kutekeleza ajenda hii ya Miji Mipya" alimalizia Mkurugenzi Mtendaji huyo wa UN-HABITAT, Bi. Maimuna Mohamed Sharif.
Aidha, Mawaziri hao pia walipata wasaha wa kujadili kwa kina agenda hiyo ya Miji mipya ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's).
0 Comments