Header Ads Widget

MFALME ZUMARIDI ASOMEWA MAELEZO YA KESI YAKE

 


Diana Bundala maarufu kama Zumaridi na wenzake nane wameanza kusomewa maelezo ya awali ya kesi namba 11 inayowakabili ya kuwashambulia askari polisi na kuwazuia kutekeleza majukumu yao.


mbele ya Hakimu Mkazi  Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Monica Ndiyokobora, Wakili Mwandamizi wa Serikali,  Emmanuel Luvinga ameiambia mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza kuwa Mashahidi 20 wanatarajiwa kutoa ushahidi wa kesi hiyo pamoja na vielelezo vitatu kuwasilishwa mahakamani hapo vikiwamo amri ya mahakama ya Mkuyuni iliyotolewa kwa ajili ya kumfuata mtoto wa mshtakiwa namba sita aliyekuwa nyumbani kwa mfalme Zumaridi, kibali cha mahakama ya Mkuyuni pamoja na fomu ya polisi kwa ajili matibabu ya askari Mgaya PF 3.


Aidha wakili Luvinga ameiambia mahakama hiyo kuwa kesi namba 12 inayomkabili Zumaridi na wafuasi wake 93 imeshindwa kutolewa maelezo ya awali kufuatia washtakiwa wawili kutofika mahakamani kutokana na changamoto ya kiafya huku kesi namba 10 inayomkabili Zumaridi ya usafirishaji haramu wa binadamu ikiwa upelelezi wake ukiwa bado haujakamilika.



Kutokana na hatua hiyo, hakimu Monica Ndyekobora amepanga kesi hiyo hadi Mei 12 mwaka huu washtakiwa hao watakaporudishwa  mahakamani hapo kwa ajili ya kusomewa  maelezo yao ya awali.


Tangu Zumaridi na wafuasi wake 93 walipokamatwa hadi sasa wafuasi watano pekee pamoja na Zumaridi bado wanaendelea kusota katika gereza kuu la Butimba huku wengine wakiwa nje kwa dhamana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI