Header Ads Widget

DC WA MBEYA ATAKA VYOMBO VYA USAFIRI KUWATAZAMA WENYE ULEMAVU


Na Matukio daima media ,Mbeya

SERIKALI wilaya ya Mbeya imevitaka vyombo vya usafiri wa umma na wadau kuwasaidia watu wenye ulemavu kuwavusha kwenye vivuko vya watembea kwa miguu kwenye miundo  mbinu ya barabara pindi panapokuwa na uhitaji .

Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Mbeya,Dkt. Rashid Chua Chua wakati akizungumza na mtandao huu  ofisini kwake juu ya mikakati ya serikali katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ambao wamekuwa wakikumbana na changamoto ya kuvuka barabara .


Dkt. Chua chua amesema kuwa jambo hilo watu wa vyombo vya usafiri wanaliweza ,lakini pia kunaweza kukawa na changamoto kwenye daladala na vitu vingine  hivyo amewaomba wananchi wa  mbeya kuwasaidia kuwapindanisha kwenye daladala watu wenye ulemavu wasiojiweza .


“Nitoe kwa jamii kuguswa kwa wenzetu hawa wenye ulemavu ambao wanaonekana kuwa mtihani huu kwani nao hawakupenda kuwa hivyo , maana kuna muda mwingine dereva wa dala dala  na mabasi makubwa anaweza akawa anaendesha lakini akaona kazi kusimamisha gari sababu mlemavu anavuka hivyo tunaomba wawe na huruma kwa wenzetu hawa “amesema Dkt. Chuachua.


“Ukifika kwenye suala la kuvuka barabara watu wenye ulemavu wanakuwa katika wakati mgumu sana ,wiki iliyopita nikiwa napita maeneo ya barabara ya hospitali ya rufaa nilikuta mlemavu mmoja anavuka barabara kwa kutambaa kwa shida kwakweli niliumia sana ikabidi nimwambie dereva asimame na nikamsaidia ''amesema.




''Sasa tuna mpango kwenye makutano ya barabara kuu ya kwenda eneo la Sokomatola watahakikisha kunakuwa  na  alama zote za barabarani  zinazohusu watu wenye ulemavu na watembea kwa miguu  pamoja na baiskeli  za miguu mitatu na kutakuwa na uangalizi wa kipekee.


Hata hivyo Dkt. Chua chua amesema kuwa pia watahakikisha maeneo yote yanayojengwa barabara katika jiji la mbeya ili watu wenye ulemavu waweze kuzitumia barabara hizo kiurahisi zaidi .


Kwa upande wake Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti  wa Usafiri ardhini (Latra),Denis Daudi amewataka wamiliki wa vyombo vya moto na madereva mabasi ya Mama kuzingatia sheria za usalama barabarani kwenye maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu


“Asilimia kubwa eneo hili wahusika wakuu ni wenzetu polisi   wanatakiwa kusimamia kikamilifu kwa kuhakikisha  wenye magari kuzingatia sheria za barabarani na kuona wenzetu wenye ulemavu  walizaliwa i tulio wazima tusijisahau sanaa maana hatujui kesho yetu”amesema Daudi .


Thabitha Bughali Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali  la Sauti ya Mama Afrika (Samofa) ambalo linahusisha na kusaidia makundi maalum amesema kuwa upo muhimu kwa madereva na wadau kuwasaidia watu wenye ulemavu pindi wanapokuwa wanavuka kwenye vivuko vya barabara.


“Mara nyingi huwa nashuhudia jinsi watu wenye ulemavu wanavyopata shida nyakati za kuvuka barabara mvua ikiwa inanyesha ndo huwa changamoto zaidi kwao maana muda mwingine anatumia hata nusu saa kuvuka maana ulemavu wao upo tofauti hivyo tunapaswa kuwasaidia watu hawa “amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI