Na Matukio Daima APP, Liwale
Baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na tano vimeteketezwa Wilayani Liwale Mkoani Lindi baada ya muda wake wa matumizi kuisha.
Mkaguzi wa dawa kanda ya kusini Elias Nyaonge kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) alisema kuwa zoezi hilo limefanywa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
Aidha amefafanua kuwa uteketezaji huo umefanyika katika hospitali ya Wilaya ya Liwale kupitia idara ya Afya baada ya kupata kibali kutoka kwa mhakiki mali wa Serikali ili zoezi hill liweze kufanyika.
"Katika uteketezaji huo sehemu kubwa ya vifaa vilikuwa ni sindano, gloves, mipira ya kiume na vingine vichache vilivyokuwa vinatumika hospital, vituo na zahanati pamoja na maduka ya dawa"
"Ni vema halmashuri zingine zikaiga mfano ili kuhakikisha wanateketeza bidhaa ambazo zimeisha muda wake kwa mujibu wa sheria na kuafuata tararibu zilizowekwa kwenye mwongozo bila kukiuka" alisema Nyaonge
0 Comments