Na mwandishi wetu, Tandahimba
Benki ya CRDB imeongeza neema kwa Benki ya wananchi Tandahimba TACOBA kwakuzindua huduma za uwakala katika benki hiyo ambapo zaidi ya 8774 wanatarajia kunufaika na huduma hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya uwakala wa benki ya CRDB kwenye Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) Meneja wa Mkuu wa benki hiyo Yahaya Kiyabo alisema kuwa sasa wanaweza kuwafikia wateja wengi zaidi kwakutumia huduma za uwakala.
“sasa ni kama tumezindua matawi 20,000 kitu ambacho kwetu lingekuwa jambo gumu lakini kwa CRDB iliwezekana na pia waliwekeza zaidi ya Bil. 3.1 ili kutukwamua kwenye changamoto ya mtaji ambapo kufikia mwaka 2021 tulirekodi faida ya shilingi 139 ikiwa ni ongezeko la shilingi 235 ukilinganisha na faida tuliyorekodi mwaka 2020” alisema Kiyabo
Nae Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa benki ya CRDB Ericky Willy alisema kuwa katika mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma sasa wanaweza kutumia benki ya tacoba kupitia matawi ya CRDB benki.
“sisi tuna mawakala zaiid ya 800 lakini kwa mkoa wa Mtwara kwa tandahimba tunao mawakala 170 ambapo tunaamini kuwa TACOBA sasa itasambaa zaidi” alisema Willy
“Tacoba wanamafanikio makubwa kwakweli wameupiga mwingi nikiwa kama mkuu wa kitenge cha huduma niwahakikishie hampaswi kuwa na wasiwasi kwetu kupitiia huduma hii na nyingine tutawapa fursa ya kupata huduma kwa uhakika zaidi”alisema Willy
0 Comments