Header Ads Widget

WANAWAKE WATAKIWA KUFICHUA VITENDO VYA UNYANYASAJI

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Katibu Msaidizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Salvatory Kaiza amewata watumishi wanawake kutoka katika taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu kukemea na kufichua vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika mafunzo ya nidhamu na utaratibu wa undeshaji wa mashauri ya nidhamu sehemu za kazi yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU)- wanawake Taifa.



Amesema kuwa, kumekua na malalamiko kwa watumishi wa umma juu ya kucheleweshewa maamuzi yao kutokana na watu wanaopeleka mashauri hayo kutokamilisha vielelezo vyao, hali inayopelekea mashauri hayo kukaa kwa muda mrefu.


"Nidhamu ni suala la muhimu sana kwa watumishi wa umma ili kufikia malengo ya taasisi, ni vyema wafanyakazi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni mahali pa kazi ili kufanikisha utendaji wa kazi katika taasisi,kulinda utumishi wetu na tumalize utumishi wetu salama pia kuwalinda watoto wetu hasa wa kike waliopo vyuoni" amesema Kaiza.




Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Eventus Mugyabuso amesema pindi mtumishi wa umma anapoachishwa kazi, mwanamke ndiye mhanga mkuu, hivyo ni jambo jema kuwepo kwa mafunzo ya nidhamu mahala pa kazi.



Naye, Kaimu Mratibu Msaidizi kamati ya wanawake THTU, Roselyne Mathew Massam amesema, mafunzo hayo yameratibiwa na Chama cha Wanawake THTU kuelekea kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yenye lengo la kusaidia watumishi kuelewa umuhimu wa nidhamu mahali pa kazi, kupunguza migogoro kazini na ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.




Aidha,amesema Tume ya Utumishi wa Umma kuongeza wafanyakazi wanaoshughulikia mashauri ya nidhamu sehemu za kazi ili kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.


"Tunaomba tume iongeze watendaji ili kusaidia kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi,mashauri mengi yanachukua muda mrefu na inachukua muda mrefu kwa mfanyakazi kurudishwa kazini" amesema Roselyne.



Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na wanawake wa THTU kuelekea kilele cha Siku wa Wanamke Duniani Machi 8, 2022.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI