Na chausiku Said _ Mwanza.
Meneja wa shirika la umeme (Tanesco) Mkoa wa Mwanza Felix Olang amewataka wananchi kupenda kuangalia na kusikiliza vipindi vinavyorushwa na shirika hilo ili kuepukana na majanga ya moto yanayotokea pamoja na malalamiko ya kuibiwa wakati wa kupelekewa huduma hiyo.
Akizungumza na Matukio Daima ameeleza kuwa wananchi wengi Hawapendi kufatilia elimu inayotolewa na Tanesco namna ya kujikinga na majanga ya moto wengi wao wanapenda kuangalia tamthilia na mpira.
Olang amesema kuwa Tanesco wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia usalama wa wananchi na mali zao .
"Hata kama utatulipa mabilioni ya pesa kama hakuna usalama kwenye nyumba yako au kiwanda yani mahari popote unapoweka umeme ni bora ukabaki na pesa zako"alisema Olang.
Amefafanua kuwa Tanesco wanatumia pesa nyingi kuhakikisha elimu ya usalama na majanga ya moto majumbani inawafikia walengwa ipaswavyo katika jamii.
" kitu ambacho ningeomba wananchi wajaribu kuangalia vipindi vya elimu vinavyotolewa na Tanesco kwenye tv na radio wakati mwingine tunaweka matukio pamoja na miradi mbalimbali inayofanywa na tanesco"alisema Olang.
Ameeleza kuwa kutokana na elimu wanayoitoa na wananchi kutosikiliza baadhi ya watu wamekuwa wakipeleka malalamiko ya kuibiwa.
"Ukifika wakati wa vipindi vya tanesco wakina mama wanahamisha channel wanaona ni bora kuangalia tamthilia na wakina baba wanaangalia mpira wa ulaya" alisema Olang.
Tanesco hatuhusiki na ufungaji wa waya Majumbani kwa sababu sheria haituruhusu kuna makandarasi ambao wamepewa leseni na serikali na wanatambulika kisheria hao ndio wanadhamana ya ufungaji ya waya kwenye nyumba ya mteja.
Pia tanesco tunadhamana ya kuangalia mtu aliyehusika na ufungaji wa waya amefunga kuendana na kiwango cha leseni yake aliyopewa na ewura na kuangalia kama ameweka kithibiti umeme.
Aidha ameeleza kuwa kuna ulazima wa kila miaka mitatu mtu kufanya marekebisho ya nyaya za umeme katika nyumba anayoishi.
0 Comments