Na mwandishi wetu, Mtwara
Taasisi ya utafiti wa kilimo TARI kituo cha Naliendele mkoani Mtwara wameweka mazingira ya kumuwezesha mkazi wa mkoa wa Mtwara atakae Lima zao la migomba kupata shilingi milioni 27 ndani ya mda mfupi katika eneo dogo la ardhi ambapo Miche ya migomba ya kufanikisha mapato hayo imeanza kuzalishwa kwenye taasisi hiyo.
Akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Chuo cha Kilimo Borigaram - Kigamboni waliotembelea taasisi hiyo kujifunza kwa vitendo ambapo ,
Mkurugenzi wa TARI kituo cha Naliendele Dr. Fortunus Kapinga alisema kuwa taasisi imeona Bora kuwawezesha maarifa na mbegu Bora za matunda ikiwemo ndizi kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara ili waweze kukidhi mahitaji ya soko bila kutegemea mazao hayo kutoka nje ya mkoa.
“Tafiti za kilimo cha mboga na matunda(hotculture) wanafunzi hao wamesema wameshangaa kuona migomba ikisitawi na kuzaa kwa wingi na kudai kuwa wakazi wa Mtwara wanaweza kutengeneza kipato kikubwa wakati wakisubiri mavuno ya korosho” alisema Kapinga
“Ekolojia ya Mtwara inaruhusu wakulima wa Mtwara kulima mazao mengi yakiwemo mazao ya bustani, jamii ya kunde na nafaka bila kuathiri kilimo cha zao la korosho ndio maana tumeamua kutoa elimu ili wakulima waweze kujiongezea kipato kutoka kwenye mazao hayo badala ya kutegemea zao la korosho peke yake”
0 Comments