Na Mwandishi wetu, Kigoma
Kutokana na uhaba wa mafuta ya kula nchini Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Geoffrey Mkamilo amekuja na staili mpya ya kutumia mikutano ya hadhara kuhamaasisha wananchi mkoani Kigoma kulima zao chikichi kwa kutumia mbegu mpya aina ya Tenera iliyofanyiwa utafiti na taasisi hiyo kituo cha Kihinga.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lugongoni na kandaga Wilayani Uvinza alisema kuwa wananchi wanapaswa waelimishwe na wahamasishwe ili kuisaidia serikali kupungiza gharama kubwa inayotumika katika uagizaji wa mafuta ya kula nchini.
Alisema kuwa taasisi hiyo inategemea kuanzisha vitalu katika vijiji ili kuwezesha wakulima kupata mbegu hizo kwa urahisi na kuwaondolea usumbufu wa kufata mbegu hizo katika kituo cha Kihinga.
Nae Abiudi Obeid mkazi wa vijiji cha Kandaga alisema kuwa TARI iangalie namna ya kuwasaidia wakulima kupata mbegu hizo kutokana nanchangamoto ya usafiri mpaka mbegu hizo kuwafikia.
“Sisi tunakushukuru Mkurugenzi Mkuu wa TARI kwa ujio wako hapa kijijini kwetu. Kwa kweli uhamasishaji ni mdogo sana nfio maana wakulima wengi hawajahamasika bado tunatumia mbegu za michikichi ya zamani ujio wenu unaweza kuwa chachu ya kufanya mabadiliko katika zao hili” alisema Obeid
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Hanali Msabaha alisema kuwa wamejipanga kuendeleza zao hilo kwa kuanzisha vitalu vya mbegu ambazo zitawasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa chikichi katika wilaya hiyo.
Alisema kuwa Wilaya ya Uvinza Ina jumla ya vitalu 33 ambavyo vinamilikiwa na makundi mbalimbali ya wakulima, Taasisi za dini, Shule za msingi na sekondari ambapo mahitaji ya mbegu zilizootoshwa zilifikia zaidi ya 1,500,000
0 Comments