Na, Titus Mwombeki-MTDTV.
Wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ambao wameonekana kusuasua katika ulipaji wa Kodi mbalimbali wametakiwa kuacha tabia hiyo haraka na kuanza kulipa kodi na tozo wanazotakiwa kulipa kwani wasipofanya hivyo sheria itachukua mkondo wake.
Hayo yamesema na mkuu wa wilaya ya Manispaa Bukoba Moses Machali alipokutana na wafanyabiasha wa manispaa ya hiyo katika ukumbi wa Bukoba sekondari ili kutoa elimu juu ya Kodi na tozo mbalimbali na kusema kuwa wamekuwepo baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikahidi kuulipa kodi zikiwemo za ulipaji wa ushuru wa huduma.
"Kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiashara ambao wanakahidi kulipa Kodi na tozo mbalimbali zilizowekwa na serikali mpaka tusukumane, serikali atupende kutumia nguvu ila kama mtu anapewa wito zaidi ya Mara tatu na atokei tutamkamata tu"
Aidha amewata maafisa wa serikali wanaohusika na ukusanyaji wa kodi mbalimbali ndani ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba kutumia lugha nzuri na kutotumia nguvu wakati wakitekeleza majukumu yao ya ukusanyaji wa kodi.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Hamid Njovu amesema kuwa furaha ya serikali ni kuona wafanyabiashara wakiendelea kufanya biashara zao zikikua sio na sio kuona wakifiridhika.
"Kuna baadhi ya sheria ambazo haziwezi kuchezewa na mtu mfano yoyote mfano Leseni ya biashara hiyo uwezi kusema chochote kwani nikibali cha mfanyabiashara Katika eneo husika lakini Kuna baadhi ya sheria ambazo labda tulizitengeneza Miaka iliyopita zinakuwa kero Kwa mfanyabiashara miaka hii hizi tutanaweza kuziangalia upya ili tubaki na sheria za msingi tu zinazoendana na miaka hii"
Kwa upende wake meneja msaidizi kitengo cha ulipaji wa kodi na madeni mkoa wa kagera Elias Joseph Huruma amewashukuru wafanyabiashara mkoani kagera kwani wamekuwa wakijitahidi kulipa kodi na kuwaomba kuendelea hivyo kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mashine za EFD ili kuongeza mapato ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
"Wafanyabiashara mkoani Kagera wamekuwa wakijitahidi sana kulipa Kodi na tunawashukuru Sana Kwa Hilo, niwasihi waendelee kuzingatia matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD mashine) wanapokuwa wanakifanya shughuli zao za kibiashara na hii itawezesha mkoa wetu kuongeza mapato"
Naye Deus Alexander mfanyabiashara manispaa ya Bukoba amewashukuru viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Kutoe elimu kwao na kuwaomba yale waliyoahidi kwao ikiwemo kutazama upya baadhi ya sheria ambazo zimeonekana kuwa kandamizi kwao kuangaliwa upya na Kwa haraka zaidi.









0 Comments