Header Ads Widget

VIKUNDI 18 VYA UZALISHAJIMALI VYA WANAWAKE ,VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WAKABIDHIWA VIFAA VYA MIKOPO VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MIL.104

 


HALMASHAURI ya Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Kupitia asilimia 10 ya  mapato ya ndani imekabidhi vifaa/ mikopo yenye thamani ya Sh. Zaidi ya Milioni 104 kwa vikundi 18 vya uzalishajimali vya wanawake ,vijana  na watu wenye ulemavu  ili kuviwezesha  kujikwamuwa  kiuchumi.


Akikabithi mikopo hiyo  Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani  humo Mwanahamisi Munkunda  amewataka wanawake kutumia Fedha hizo kwa lengo lililokusudiwa Na si vinginevyo .


‘’Wanawake wengi ni waaminifu lakini wanashindwa kurudisha mikopo kutokana akishatoka kuchukua  mkopo akifika nyumbani  baba anamwambia lete hiyo hela kuna dili Fulani nikalipige nitapata hata milioni nane mwishowe anashindwa kurudisha rejesho  na hela anaenda kuolea mke wa pili hiyo ndo changamoto kubwa ,’’ alisema Mkuu huyo.



Pamoja Na hayo Munkunda amewata Wajasiriamali hao kuchamkia Fursa zilizopo katika wilaya hiyo ikiwemo minada za kila Mwezi za wilaya, Kilimo cha mpuga ili kuhakikisha  wilaya hiyo iinajitambulisha  kwa kuwepo kwa  kitu cha tofauti Na cha pekee .


Awali akiwasilisha taarifa ya mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya jamii ya wilaya ya Bahi  Denis Komba amesema  changamoto zilizopo ni pamoja Na madeni Sugu kwa baadhi ya Vikundi kutorejesha mikopo kwa wakati hasa vikundi vya vijana na watu wenye ulemavu Na kudai kuwa jitihada za ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa kuvitembelea ilimkuangalia uhai wa miradi yao na mipango yao juu ya ulipaji wa deni.




Naye Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Bahi  Stewart Masima  amewataka  wajasiriamali Hao kubadili Fikira Na kuacha kufanya biashara kwa mazoea na matokeo yake wajipambanue ili kuweza kuibadilisha wilaya hiyo kiuchumi .


Nao Baadhi ya Wajasiriamali waliopokea Mikopo Na vifaa hivyo akiwemo Deogratius John mhasibu kikundi cha TUNAWEZA WALEMAVU Bahi Makulu wameishukuru  serikali ya  awamu ya sita  kwa kuwajali  watu wenye uhitaji  Na kuwataka wajasiriamali wenzao kufanayakazi kwa bidii na kuiomba tena Serikali   kuwatafutia masoko ili Bidhaa wanazozidhalisha ziweze kuuzika kwa lengo la kuzisaidia familia zao ziweze kupata mahitaji ya Msingi ikiwemo kusomesha Watoto.



Kupitia fedha za marejesho Halmashaurikwa kipindi cha mwaka wa utekelezaji imewezesha jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi Zaidi ya milioni 118,kwenye jumla ya vikundi 26 aidha kiasi cha Shilingi Zaidi ya milioni 13 zilikopeshwa robo ya kwanza

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI