Header Ads Widget

TUNACHOKITAFUTA SIO MADARAKA NI KHATMA NJEMA YA ZANZIBAR - MHE. OTHMAN



Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman, amesema thamani ya visiwa vya Zanzibar ni kubwa kuliko madaraka ya uongozi ndani ya nchi.


Mhe.Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  ameyasema hayo Machi 12, akizungumza na wanachama wa chama hicho jimbo la Makunduchi, katika muendelezo wa ziara yake ya kiuimarisha chama katika majimbo ya Zanzibar.



Mhe. Othman amesema wako baadhi ya watu hupigania nafasi za uongozi hata kwa njia ambayo si sahihi bila kujua thamani ya Zanzibar  kuwa ni kubwa kulikoni madaraka wanayoyapigania.


Alisema Zanzibar ilikuwa kitovu  cha uchumi  Barani Afrika lakini leo ubora huo umepotea kutokana na baadhi ya watu kupigania maslahi binafsi na kuacha mustakbali wa nchi.



Othman alieleza kuwa zanzibar ina fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinaweza kusaidia kuondoa changamoto ya ajira kwa vijana na umasikini kwa ujumla ikiwa viongozi watasimamia hilo kwa maslahi ya nchi.


Akizitaja fursa hizo Mhe. Othman amesema Bahari,Utalii na sekta ya mafuta na gesi ni vyanzo vikubwa vya utajiri wa Zanzibar kama viongozi watazingatia uwajibikaji, uadilifu na uaminifu katika kusimamia rasilimali hizo.



Katika ziara hiyo ya kuimarisha chama Mhe. Othman alipata fursa ya kuweka Jiwe la msingi na kupachika bendera katika tawi jipya la chama hicho la ‘KIJINI MAKUNDUCHI’ katika shehia ya kijini Makunduchi.


Aidha Mh. Othman aliweza kutembelea Shamba la Nyanya na Midimu katika eneo la Bwejuu katika Jimbo la Paje Mkoa wa kusini Unguja na kujionea chamoto mbali mbali ikiwemo ndimu nyingi kukauka kutokana na kukosa soko na kutokuwepo kwa miundombinu ya umeme ambao unahitajika sana katika kumwagilia maji mazao hayo, pamoja na kumuombea dua marehemu Ameir bin Soud bi Ameir (Bindu) katika makaburi yao huko Bwejuu,kabla ya kumalizia mkutano na wanachama wa chama hicho jimbo la Paje.



Katika ziara hio Mhe. Othman aliambatana na viongozi mbali mbali wa chama hicho wakiwemo Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar, Ndg. Salim Biman, Mshauri wa Chama Ndg.Juma Said Sanani, Wajumbe wa Kamati Kuu Ndg. Ismail Jussa, Hamad Mussa Yusuf na Hassan Jani Masoud,  Mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Chama hicho Mohamed Khamis (Edy Calipso), Katibu wa Ngome ya Wazee Taifa Bi.Arafa Mussa Uledi na viongozi wa taskfosi ya Ngome ya Wanawake wa chama hicho.


Ziara hio itaendelea tena hapo kesho tarehe 13/03/2022 kwa majimbo ya Malindi na Chumbuni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI