Header Ads Widget

NAENDELEA KUJISHIKA KICHWA

 



Adeladius Makwega-DODOMA


Asubuhi ya Machi 11, 2022 Shirika la Utangazaji la Ujerumani-DW Kiswahili lilirusha hewani Makala ya Sura ya Ujerumani iliyobeba maudhui ya taifa hilo namna lilivyobadilisha Sera yake ya Usalama na Kujilinda, baada ya Mgogoro wa Urusi na Ukraine unaolindima.


Makala haya yaliandaliwa na waandishi wawili wa Peter Hills na Nina Vick Hozer huku yakisimuliwa na mtayarishaji Alison Mwilima wa DW Berlin, yalitwikwa kichwani cha habari cha dhana ya mabadiliko ya kibajeti na mabadiliko makubwa ya tekinolojia katika mapambano ya kijeshi.


Japokuwa Makala haya yanalipuliza zumari hadharani kwa kumjengea hoja msikilizaji kutambua namna Ujerumani inavyojizatiti kuwa na jeshi bora na imara barani ulaya lakini ndani yake yanajenga picha nyengine kwa msikilizaji wa mataifa ya ulimwengu wa tatu kuwa lipi la kufanya kwa mataifa yao.


Huku ikiibua dhana ya gere kwa msikilizaji huyu dhidi ya taifa hilo.


“Mbona wenzetu wanakwenda mbali sana.”


Makala haya yamenipa mwanya wa mimi kuyatafakari maboresho hayo ya Jeshi la Ujerumani.Ifahamike wazi kuwa Ujerumani iliathirika mno na vita vya pili vya dunia na mara baada ya hapo ilichukua hatua kadhaa ambazo leo hii inaliweka pahala pazuri na ndiyo maana wapangaji wa sera za taifa hilo jambo hili waliliona mapema kabla ya Mgogoro wa Urusi na Ukraine. 


Mikakati hii imekuja kutokana na Ushirikiano wa Kijeshi wa Ujerumani na Marekani, kwani uwepo wa kambi ya kijeshi za Marekani nchini humo ni ishara tosha kuwa anayemchokoza Mjerumani amemchokoza Mmarekani.


Hapa ni sawa na kuku na bata ambao wapo katika nyumba kimoja na wote wametaga mayai yao, pale anapokuja mharibifu na kutaka kuharibu /kudokoa mayai yaliyomo ndani ya banda ni wajibu wa kuku na bata kupambana kwa pamoja hadi kumdhibiti mharibifu huyo ili mayai yao yawe salama. 


Hayo ni matokeo ya Kambi ya Kijeshi za Marekani kama ya Ramstein iliyopo Kusini Magharibi mwa Ujerumani. Kambi hii ndiyo kambi kubwa na Makao Makuu ya Jeshi la Marekani kitengo cha Jeshi la Anga kwa Ulaya na Afrika huku pia ikiwa ni kamandia ya NATO.


Kambi hii ya Ramstein ipo umbali wa Kilometa 16 kutoka mji wa Kaiserslauter Wamerakani wanalitambua eneo hilo kama K TOWN na lilijengwa kati ya mwaka 1949-1953 mara baada ya vita vya pili vya dunia kwisha nakuanza kazi mwaka rasmi mwaka1953 hadi leo.


Mtangazaji Allison Mwilima katika makala haya, amejenga dhana ya kambi hiyo kwa miungurumo ya ndenge kadhaa za Kimarekani zinazovyoruka angani, akijenga picha ya ndege hizo za F 35 zinavyooneka kwa yule anayezitazama kama vidoti viwili vyeusi huku zikiongezeka ukubwa zinavyokaribia ardhini. Sauti hizo zikionesha kweli makala hayo yanaonesha uso wa Ujerumani wenye jeshi bora.


Kama hilo halitoshi taswira ya dolia kwenye mpaka wa Ukraine na Poland huku Urusi na Ukraine wakipigana ilielezwa.


Makala haya yalitaja ununuzi wa ndenge za F 35 za kuziweka kando ndenge za awali za Tornado za mwaka 1970 ambazo bado zina uwezo mkubwa lakini zinawekwa kando ili jeshi la Ujerumani kwenda na wakati.



Utafiti wa manunuzi wa ndenge hizo unakadaliwa ndege moja inagharimu dola milioni 78 ambayo ni sawa na Tsh.180,648,000,000/= (bilioni Tsh180.7/=). Hilo likiambatana na manunuzi ya ndege kadhaa zisizo na rubani kutoka Israel.


Orodha hiyo ya mabadiliko ya kijeshi pia imeelekezwa katika mfumo wa Combart Air System ambayo Wajerumani wenyewe wanashirikiana na Wafaransa kuwa na ndege bora katika mapambano katika uwanja wa kivita na kuboresha Hedikopta zao kuwa na uwezo wa kubeba mizigo mizito.

Makala haya yalitaja bajeti ya Euro bilioni 100 zilizoongezwa katika bajeti ya mwaka 2022 sawa na Tsh.252, 770, 000, 000, 000/=. Kiasi hicho cha trilioni Tsh 252 na biloni 770, wakati bajeti nzima ya mataifa mengi ya dunia ya tatu kinaingia kati ya mara saba hadi kumi kwa bajeti ya mwaka.


Kumbuka tu msomaji wa matini haya kuwa hiyo ni bajeti ya nyongeza tu huku bajeti halisi ya kila mwaka ikiwa ni euro bilioni 47.


Makala haya ya Sura ya Ujerumani yanaweka milango wazi ya darasa kwa vyama vya siasa kuwa japokuwa chama cha siasa kinaweza kuwa na mtazamo A katika jambo fulani lakini mtazamo huo unaweza kuwa B kutokana na mazingira kadhaa yanalolikabili taifa. Kwani hapa chama cha mlengo wa kushoto cha SPD awali kilikuwa kinapinga kuongeza fedha katika bajeti ya jeshi lakini kikapindua meza na kukubadili sera ya ulinzi wa taifa hilo. 


Makala haya yamemnukuu Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akisema kuwa wanahitaji ndege zinazoruka, meli zinazoweza kutumwa maeneo mbalimbali, askari wao wenye vifaa bora katika misheni mbalimbali za kivita kwa kuwalinda Wajerumani na kuilinda Ulaya.


Binafsi naona kuwa ongezeko hilo la bajeti katika jeshi hili nia yake ni kuwa taifa moja linajiweka kuwa bora na kuweza kupambana na yoyote yule atayajaribu kulichokoza.


Swali ni je mataifa masikini ya ulimwengu tatu na yenyewe yapange foleni kununua ndege za F 35? Mataifa haya yakae kimya tu kwa kujishika vichwa wakati maboresho haya ya vifaa vya kijeshi yakifanyika huko Ulaya na Marekani? Yatazame tu ruling zao namna madege makubwa yakiruka vitani kama senema na michezo ya kuigiza? Yachague upande wakuunga mkono wa mataifa haya makubwa ili yaweke kambi zao za kijeshi katika mataifa yao huku dhana ya mgeni njoo mwenyeji apone itatamalaki?


Mimi naendelea kujishika kichwa, huku nikiwashukuru mno Peter Hills, Nina Vick Hozer na Alison Mwilima wa DW kwa kuibua hoja hiyo mawazoni mwangu


Nakutakia siku njema


makwadeldius@gamail.com

0717649257

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI