Header Ads Widget

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUREKEBISHA SHERIA YA WATU WENYE ULEMAVU.

 


Na THABIT MADAI, ZANZIBAR


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga kurekebisha Sheria namba 9 ya mwaka 2006 ya Watu wenye Ulemavu ili kuendana na Mahitaji ya Wakati kwa Watu Wenye Ulemavu Nchini.


Kauli hiyo imetolewa na aliekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza Rais Sada Mkuya Salum ambapo Amesema kuwa Kutokana na Sheria hiyo kuwa ni ya Muda Mrefu sana ni muhimu kurekebishwa Mapungufu yaliyojitokeza katika kuwahudumia na kuwawezesha Watu Wenye Ulemavu Kulingana na Wakati Uliopo.


“Kuna Mapungufu Mengi yamejitokeza katika kuwahudumia Watu wenye Ulemavu Nchi hivyo Wakati umefika kwa Serikali kufanya Marekebisho ya Sheria Namba 9 ya mwaka 2006 ya Watu wenye Ulemavu,” alisema.


Waziri Sada ambaye kwa Sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar akitaja Miongoni mwa Mapungufu hayo ni kama vile Serikali kuweka Muongozo wa Miundombinu Rafiki ya Majengo ya Umma kwa Watu wenye Ulemavu lakini bado kuna baadhi ya taasisi za Serikali na binafsi hazijazingatia muongozo huo jambo ambalo huwasababishia usumbufu na kujiona hawana haki ya kutumia majengo hayo.


Nae Mkurugenzi wa Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAUZA) Juma Salim Ali ameeleza amewaomba Waandishi wa Habari Nchini kuibua Matatizo zaidi yanayowakabili Jumuiya za Watu wenye Ulemavu.


“Katika Jamii zetu kuna changamoto nyingi zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu pamoja na Jumuiya zinazowasimamia hivyo niwaomba Waandishi wa Habari kuibua Matatizo yanayowakabili,”alieleza.


Katika Hatua nyingine alieleza kwamba Watu Wenye Ulemavu bado wanakabiliwa na Changamoto ya kuitwa majina ambayo yanwadhalilisha Utu wao pamoja na Changamoto ya Unyanyapaa dhidi yao 


Baada ya Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Zanzibar Waziri Sada Mkuya Salum ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar.

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI