Mahakama ya rufaa ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Iringa imetoa maamuzi katika shauri la rufaa No. 31 la mwaka 2020, rufaa hii ilikuwa baina ya Isaya Msofe (mkata rufaa) dhidi ya Jamuhuri.
Katika maamzi ya mahakama ya
rufaa imeamuru mleta rufaa kwamba rufaa yake imeshindwa na ameamuliwa kutumikia
kifungo cha maisha jela.
Mwenendo wa kesi hii ulikuwa
kama ifuatavyo; awali mkata rufaa Isaya
Msofe alishitakiwa na Jamhuri katika wilaya ya Mufindi tarehe 08/03/2019 kwa
kosa la ulawiti (unnatural offence) kinyume na kifungu cha 154(1)(a) cha sheria
ya kanuni za adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2012 kwa wakati huo na sasa ni
marejeo ya mwaka 2019.
Mshitakiwa alipatikana na
hatia katika mahakama ya wilaya ya Mufindi na mahakama hiyo iliamuru atumikie
kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo la kulawiti mtoto mdogo mwenye umri wa
miaka 15.
Mshitakiwa hakuridhika na
adhabu hiyo hivyo alikata rufaa katika mahakama kuu ya Tanzania Iringa na
kusikiliza rufaa yake na mahakama kuu ilitoa uamuzi kwa mkata rufaa kutumikia
kifungo cha miaka 30 jela, Bwana Isaya Msofe hakuridhika, hivyo aliamua kukata
rufaa katika mahakama ya rufaa ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga
hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania, na upande wa jamuhuri haukukubaliana na
rufaa yake ulipinga na kudai kuwa mahakama kuu ya Tanzania ilikosa hukumu yake
ya miaka 30 jela na kukubaliana na hukumu ya mahakama ya wilaya ya Mufindi kuwa
mkata rufaa alistahili kifungo cha maisha jela hivo upande wa jamuhuri
ulipendekeza hukumu iliyotolewa mwanzo na mahakama wilaya ya Mufindi isimame, mahakama
ya rufaa ilikubaliana na hoja ya upande wa jamhuri hivo imemuhukumu mkata rufaa
kifungo cha maisha jela, ili iwe fundisho kwa jamii na watu wote wenye tabia ya
kulawiti watoto wadogo.
Pia mkuu wa mashitaka mkoa
wa Iringa Bwana Basilius Namkabe amewasihi wazazi wawe makini na watoto wao wafuatilie
mienendo ya watoto wao na wawe rafiki wa watoto wao ili hata kama mtoto akipata
shida au kufanyiwa kitendo cha ukatili awe tayari kueleza kwa mzazi.
0 Comments