MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia Jenerali Balozi Wilbert Ibuge amewataka wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kutumia fursa mbalimbali zilizopo Mkoani humo ili kujipatia MWANDISHI AMON MTEGA ,MDTV RUVUMA
Wito huo ameutoa wakati akizungumza na vyombo vya Habari Mkoani humo kufuatia kazi mbalimbali za utekelezaji wa miradi zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan .
Ibuge alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo mengi ya maendeleo katika mkoa huo hivyo Wakazi wa Mkoa huo wanatakiwa kutumia fursa za maendeleo hayo kwa kujiinua kiuchumi.
Balozi Ibuge ametaja baadhi ya miradi iliyofanywa Mkoani humo ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Namtumbo -Tunduru hadi Mangaka na barabara ya kutoka Mbinga hadi Mbambabay Wilaya ya Nyasa ambazo barabara hizo zimekuwa kichocheo cha maendeleo kwenye mkoa huo.
Licha ya mafanikio ya miundombinu ya barabara hizo amezungumzia pia mafanikio katika sekta zingine ikiwemo ya Elimu,Afya,Kilimo na Ufugaji,ambazo katika mkoa wa Ruvuma zimeendelea kufanya vizuri kwa sekta hizo kuimarishwa pamoja na kupatiwa miradi yenye tija kwa Wananchi.
Hata hivyo kwa namna ya pekee alizungumzia ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu linalounganisha Lituhi katika Wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe jambo ambalo amesema limeondoa kero iliyokuwa ikiwapata wakazi wa maeneo hayo ambao walikuwa wanakosa kiungo muhimu.
0 Comments