Header Ads Widget

NCCR- MAGEUZI KUKUTANA NA RAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA TCD

 


Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema kitashiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaotarajiwa kufanyika jijini Dodoma kuanzia Machi 30 hadi 31 mwaka huu baada ya masharti yao kutekelezwa.


Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Taifa wa chama NCCR Mageuzi , Edward Simbeye amesema wameridhia kuhudhuria Mkutano ambao utahudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Amesema kuwa, hatua hiyo imekuja mara baada ya kamati kuu ya Chama hicho kuridhia kushiriki kutokana na mapendekezo yao kutekelezwa.


Chama hicho ni miongoni mwa Vyama vitano vitakavyoshiriki katika mkutano huo  baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi juzi kuridhia kufuatia matakwa yao waliyotaka yafanyiwe kazi ili waweze kushiriki kutekelezwa.


Amesema kuwa, miongoni mwa matakwa ambayo walitaka yafanyiwe kazi ni pamoja na kutaka Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe aachiwe huru bila masharti.


Mengine ni walitaka kikao hicho cha TCD kisiitwe kongamano na badala yake uitwe ni mkutano ili vyama vya Siasa viutumie kujadiliana mambo mbalimbali na kupata muafaka.


Ameongeza kuwa,takwa jengine walitaka kabla ya kufanyika mkutano huo lazima viongozi wa vyama wanachama wa TCD wakutane na Rais Samia kabla ya kufanyika mkutano huo jambo ambali limekubaliwa kwani watakutana na Rais Machi 18 mwaka huu.


“ Kamati Kuu imesema hoja zetu zote zimezingatiwa, kwahiyo tutashiriki mkutano huo kama mwanachama halali wa TCD, amesema Simbeye.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI