Header Ads Widget

MBUNGE WA KIBAHA MJINI ATOA MSAADA WA SIMU JANJA 14 KUSAIDIA USAJILI WANA CCM KIDIGITALI

 


KATIKA kuhakikisha usajili wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanasajiliwa kidijitali Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametoa simu janja 14 kwa ajili ya usajili huo kwenye Jimbo hilo.

Koka alitoa simu hizo na kumkabidhi katibu wa CCM mkoa Said Goa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao na viongozi wa sekretarieti za kata kwenye Jimbo hilo.

Alisema kuwa wakati chama kinaelekea kuchagua viongozi wake lazima itambue wanachama wake kidigitali.

Aidha alisema kuwa kila kata itapata simu moja ndiyo sababu ameamua kuunga mkono chama kutambua wanachama wake.

Naye mgeni rasmi katika kikao hicho ambaye ni katibu wa CCM mkoa wa Pwani Said Goa alisema kuwa simu hizo zitasaidia kwenye usajili wa wanachama.

Goa alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ya mwisho kwenye usajili wa wanachama kwa njia hiyo kati ya Wilaya tisa za mkoa huo.

Alisema kuwa moja ya changamoto walizokuwa nazo ni ukosefu wa simu za kusajilia wanachama.

Naye Diwani wa Viti Maalum Selina Wilson alisema kuwa msaada huo utasaidia kwani walikuwa na wakati mgumu kujichangisha hadi kununua simu hizo.

Wilson alisema kuwa watashirikiana na viongozi wa kata ili kusajili wanachama kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM kata ya Kongowe Simon Mbelwa alisema kuwa watapita mtaa kwa mtaa ili kuwafikia wanachama wote

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI