Header Ads Widget

MANGE KIMAMBI AMWANGUKIA RAIS SAMIA JUU YA KUENDELEA KUSHIKILIWA WAFANYAKAZI WAKE WAWILI



Mange Kimambi akiwa na Rais Samia hivi Karibuni baada ya Rais kufanya ziara nchini  Marekani kwa ajili ya mkutano wa 76 wa Umoja wa Mataifa.

Na Matukio Daima, Dar.

MWANADADA Mwanaharakati Mtanzania anayeishi na kufanya shughuli zake Nchini Mareknani, Mange Kimambi maarufu kama Dada wa Taifa ametoa dukuduku lake kwa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kuendelea kushikiriwa kwa wafanyakazi wake wawili wa Mtandao wa Mange Kimambi App.




Tukio la kushikiriwa inafuatia kukamatwa hivi karibuni na Jeshi la Polisi kwa kile kilichoelezwa matumizi mabaya ya mitandao ambapo ilidaiwa kuwa walirusha maudhui ya video ya Msanii na Kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA], ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay.

Maudhui hayo yalidaiwa kuwa yalionesha Prof. Jay akiwa kitandani chumba cha wagonjwa mahututi [ICU] hali ambayo ilileta taharuki kwa ndugu wa mgonjwa, Madaktari na uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa na kupatiwa matibabu.

Mtandao huu wa Matukio Daima ndo ulikuwa wa kwanza kuripoti juu ya tukio la kukamatwa kwa wafanyakazi hao wa Mange Kimambi App zaidi ya 10, ambapo hata hivyo awali Jeshi la Polisi halikuwa wazi kusema hadi pale Mwanadada huyo kuandika kwenye kurasa wake ndipo taarifa ya jeshi ilitoka kwa umma juu ya kuwashikiria wafanyakazi 13 pamoja na vifaa vya ofisi mbalimbali zikiwemo camera, Laptop, na vingine vingi vya Kimawasiliano.

Hata hivyo Mwanadada huyo hivi karibuni aliandika juu ya kuachiwa kwa wafanyakazi wake 11 huku wengine wawili wakiendelea kushikiliwa na jeshi kwa uchunguzi zaidi ambapo wanaoshikiliwa ni pamoja na Meneja wa Mange Kimambi App, Bw. Allen Mhina ambaye ni mdogo wa Mange Kimabi pamoja na Binti wa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Clouds Media Group, Sakina Lyoka, aliyefahamika kwa jina la Rehema Lyoka maarufu kama Reytox.

Hata  hivyo, Machi 30, 2022 mtandao huu uliweza kushuhudia bandiko la Mange Kimambi kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akiandika mabandiko ya sehemu ya kwanza na pili  akilalamikia juu ya kutoachiliwa huku akimueleza Rais Samia hali inayoendelea kati yake na jeshi hilo hali inayopelekea kutoachiwa kwa wanaoshikiliwa.

Andiko la Mange Kimambi kwenda kwa Rais;

mangekimambi_

PART 1. 

‘’Shikamoo mama,

Nakuja kwako kwa unyenyekevu mkubwa sana. Mama mnamo March 9, nilitumiwa clip ya Professor Jay akiwa amelazwa hospitali Muhimbili na nikaiposti.

‘Mimi ni mtu ambae huwa natumiwa vitu sensitive kutoka serikalini miaka yote so hakikuwa kitu kigeni mimi kutumiwa clip ya sekunde 10 ya Professor Jay akiwa ICU.


Kilichotokea March 14 polisi waliwakamata wafanyakazi wangu 13,wakihisi wao ndo wamerekodi clip. Baada ya siku chache waliwaachia 11 wakabaki na hawa wawili kwenye picha. Wa kike anaitwa Rehema Lyoka ni binti wa Sakina Lyoka yeye ni mtangazaji wa kipindi, na wa kiume ni mdogo wangu, tuna share mama, yeye ndo manager.


‘Mama mimi clip zangu huwa natumiwa na wananchi binafsi tu. Hakuna mtu kwenye ofisi yangu anajua natoa wapi information. Ni wananchi wenyewe wananiletea habari.

Sasa mama toka tarehe 14 March hawa vijana wawili wako central kwa kesi ya matumizi mabaya ya mitandao. 

Mama kinachonileta kwako ni kwamba hii kesi ni kesi yenye dhamana na sheria ya nchi inasema baada ya masaa 48 either mtuhimiwa apewe dhamana au afikishwe mahakamani. 


Hapa navyokwambia polisi na mwanasheria wa serikali wamegoma kuwafikisha vijana mahakamani wala kuwapa dhamana wakidai uchunguzi unaendelea. 

Hata kama uchunguzi unaendelea ila dhamana ni haki yao ya msingi.

Mama mpaka nakuja kwako ni kwamba tumeshahangaika koooote mpaka kwa katibu mkuu wa CCM tumefika kuomba msaada juu ya hili.


Katibu kajaribu kusaidia ila wanagoma kuwapa vijana dhamana.

Mama Issue iliyopo hapa ni kwamba kina kumpata mdogo wangu wanaona kama vile wamenipata mimi so ni kama wananikomesha.


Huyo binti Rehema ni ‘collateral damage’ sababu wakimshikilia mdogo wangu peke yake itakuwa ‘too obvious’ kuwa issue yao ni mimi.

Andika Mange Kimambi katika bandiko hilo la sehemu ya kwanza.

Kwa upande wa bandiko la Pili

Soma hapa

mangekimambi

Part 2. 

‘’Na wiki iliyopita niliambiwa nitoe milioni 10 ndo wawaachie vijana kwa dhamana. Nikaja kuandika humu kuwa polisi wananiomba rushwa ya milioni 10 basi nilipoandika wanataka milioni 10 na … ikawa ndo kama nimechochea.


Mama mpaka tumewafunguliwa kesi polisi na DPP na kesi ilikuwa leo hii [Machi 30,2022], na judge alitoa ‘order’ kuwa watuhumiwa wafikishwe mahakamani ila polisi wamekaidi agizo la mahakama.

‘Imagine’ polisi wao wenyewe hawaheshimu mahakama kwenye hili swala hapo ndo mtu anapojua kuwa hii issue ni ‘personal’.

Mama nachokiomba kwako ni kama nilichokiomba kwa viongozi wengine, tunachoomba ni sheria ifuatwe, tunachoomba vijana wapewe haki yao ya dhamana.

Kama kweli Kuna kuna kosa wamefanya itajulikana mahakamani ila sio kuwashikilia kinyume na sheria ya nchi.

Nime attacha kesi tuliyowafungulia polisi na Mwanasheria wa serikali. Kesi imesikilizwa leo asubuhi ila si polisi wala si DPP waliofika mahakamani. Kama kweli hao vijana wana makosa na ushahidi wanao kwanini wasiwafikishe mahakamani ili mahakama iwahukumu?

Ila pia nimejifunza kitu mama kuna tofauti kubwa kati ya polisi na serikali. Sometimes huwa tuandhani hawa ni kitu kimoja. Sometimes huwa tunadhani serikali ndo inawatuma polisi kufanya uonevu kwa wananchi Ila hapa nimejifunza sometimes polisi na DPP wanafree style sana.

Kwa ushirikiano tunaoupata kutoka serikalini kwenye kudai dhamana ya hawa vijana uki-compare na ushirikiano anautoa ni vitu viwili tofauti. 

Tena imefika sehemu polisi wanasema kabisa si mnajitia mnajuana na watu wakubwa.

Sometimes things happen for a reason, sikuwahi kujua kuwa kuna uonevu wa kiasi hiki kwenye jeshi la polisi, hapo ni mtu kama mimi ambae nimeweka mwanasheria mzuri, nimeweza kufikisha malalamiko mpaka kwa katibu mkuu CCM na bado polisi na DPP wamegoma kufanya haki, nimewaza je mtanzania wa kawaida asie na hata na 500 si anaweza kukaa polisi mwaka mzima bila kufikishwa mahakamani?

Alimalizia Mange Kimambi katika andiko hilo.

Hata hivyo mtandao huu unaendelea kuwasiliana na Jeshi la Polisi kufahamu sintofahamu hiyo lakini harakati bado hazijafanikiwa baada ya mawasiliano kutokuwa rafiki…

ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI MPYA KWA WAKATI JIPATIE APP YA MATUKIO DAIMA INAYOPATIKANA GOOGLE PLAY STORE BURE KABISA  


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI