Header Ads Widget

KAULI YA MBOWE IRINGA LEO

 


MWENYEKITI WA Taifa wa chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema anatambua uzito wa mwanamke na ndio maana ameamua kutopumzika na badala yake kufika Katika maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani mkoani Iringa .


Kuwa wanawake wamekuwa nguvu ndani ya CHADEMA na kwake kama muasisi wa CHADEMA anatambua walioanza na wanachama wangapi miaka 30 iliyopita kwani ilikuwa ni vigumu kukusanya wanawake watano Kwa wakati huo .


Kwani alisema  baraza la wanawake wa Chadema ni baraza lenye nguvu kubwa kuliko mabaraza ya vyama vingine likiwemo la chama tawala .




Alisema baraza la wanawake wa Chadema limekuwa na nguvu kubwa pamoja na changamoto kubwa walizopitia kwenye uchaguzi mkuu uliopita  ila Bado wameendelea kupigania nchi ya Tanzania na kuifanya kuwa sehemu salama pa kuishi .


Mbowe alisema kuwa chama litaendelea kuwaheshimisha wanawake kutokana na nguvu kubwa na misingi Bora waliyokuwa nayo ya kukitumikia chama hicho .


Mbowe alisema kuwa Kwa muda wote aliokaa gerezani Dua na Sala za watanzania ndio ambazo zilisaidia na Hadi Leo hii kuachiwa Huru .


"Ndugu zangu kama mnavyotambua kuwa Kwa zaidi ya siku 200 nilikuwa nimetiwa nguvuni na vyombo vya Dola pamoja na waliokuwa walinzi wangu    Khalipan ,Adam Kasekwa  na Mohamed Ling'wenya ambao nipo nao hapa makamanda hawa wamekaa gerezani siku 577 ama wiki 82  lakini wote Kwa pamoja nazungumza Kwa niaba Yao wanawashukuru Sana"


Alisema kuwa mawakili walifanya kazi kubwa kupitia Kwa mwakilishi wao Peter Kibatala pia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vilifanya kazi kubwa Sana kuhabatisha umma na kufanya kesi hiyo kufuatiliwa zaidi .


Kuwa kupitia vyombo vya habari ulimwengu uliweza kubaini kuwa Mbowe ni gaidi kweli ama Mbowe si gaidi.


Alisema pamoja na vyombo vya habari pia jitihada kubwa zilifanywa na mabalozi wa nchi mbali mbali kufuatilia kesi hiyo usiku na mchana jambo ambalo Kwa binafsi yake anapongeza Sana na watu wengi Sasa wamepata kuijus vyema nguvu ya familia ya Chadema .


"Nililetewa Michele na Kila aina ya msaada nikiwa gerezani pamoja na fedha za kusaidia watoto wetu na familia zetu ..hakika nasema Mungu awabariki Sana na sina Cha kuwalipa zaidi ya Mimi kusimama kutetea Kila Mtanzania "


Aidha Mbowe alisema anapongeza mamlaka zote zilizofanya maamuzi ya kutoendelea na kesi hiyo jambo ambalo anapongeza kwani maamuzi hayo yamerejesha furaha yao .


"Natambua kumekuwepo na mijadala mbali mbali pamoja na taharuki ya jinsi nilivyoweza kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ambapo taharuki hii nitaijubu hapa Leo ...Kwa muda wote gerezani nilitumia muda wangu Kusali na kumuomba Mungu " alisema Mbowe 


Kuwa maandiko yanafundisha kushukuru Kwa Kila jambo ,alisema siku zote amekuwa akihubiri kuwa CHADEMA kamwe hakitakuwa chama Cha kisasi .


Alisema  upo ukatili mkubwa ambao chama chake kimefanyiwa kwenye uchaguzi ila kamwe hawatahubiri sera za chuki .


Kuwa chadema wnahubiri Amani Kwa vitendo na wataendelea kuhubiri Amani siku zote na kutaka vyombo vya Dola vilivyoshiriki kuvuruga uchaguzi huo kuacha ujasiri Kwa kuita wengine ni magaidi .


Alisema kuwa chadema ni chama Cha kidemokrasia na hakijapata kuwa chama Kibaraka Kwa chama tawala na hakitafanya hivyo .


Mbowe alisema wajibu na misingi ya chama chake kimejenga kujitegemea na kamwe hakitakuwa tayari kubebwa na watu .


"Tulikataa na hakika hatutakubali kuwa watumwa wa fedha za watu na wale wenye tamaa ya fedha hatutasita kuwaomba waende zao "


Alisema kuwa chadema hakikuudwa ili Viongozi wa Sasa kupata faida ili kipo kuona vizazi vijavyo vinakuja kufurahia matunda ya chama hicho na Katika kujenga chama hakuna Bora kuliko mwingine .


Mwenyekiti huyo alisema kumekuwepo na nguvu kubwa za kutaka chadema kife ila watambue kuwa nguvu wanazotumia kuua chama zinasaidia kukijenga zaidi chama kuliko kubomoa .


Kwani alisema chadema inaamini Katika nguvu ya umma lakini wengine  wanaamini kupitia vyombo vya dola .


"Chadema tumevumilia Sana na niwaombe wanachama tuendelee kuvumilia uonevu wowote tunaotendewa ndugu zangu watanzania mtakumbuka Tarehe 21 Aprili nilizungumza nanyi Hotuba ndani ya Hotuba hiyo nilichambua Kwa kina tofauti ya Serikali ya awamu ya tano ,uchambuzi ambao uligusa wengine waliokuwepo madarakani kusema ukweli haikuwapendeza waliokuwepo madarakani na miezi mitatu nilitiwa nguvuni hivyo natambua kuwekwa kwangu ndani ni kutokana na Hotuba yangu hiyo"


Mbowe alisema hataacha kukemea vitendo vya utekaji na kufungana ovyo na kamwe hatanyamaza kuendelea kupinga uonevu huo.



Alisema alimwandikia barua Rais Samia kuomba kukutana nae kabla hata kwenda gerezani ila hakupata nafasi ya kukutana na alishapata kuomba kukutana na Rais Hayati John Magufuli Kwa zaidi ya Mara tatu hakuwahi kujibu .



Alisema alipata kukutana Mara kadhaa na Magufuli kwenye misiba na Matukio mengine  japo alikuwa na mpango wa kumtafuta na kumweleza wazi .


"Ndugu zangu watanzania kesi yangu ilipofutwa nilipokea ujumbe kutoka Kwa Rais Samia alitaka nikutana nae haraka iwezekanavyo nakumbuka Rais pekee ambae wapinzani tulipata kukutana nae ni Jakaya Kikwete lakini nilipopata mwaliko nilipotoka gerezani niliahidi nitafika huku niliondoa uchungu niliokaa gerezani nichukue nafasi hii kumshukuru Rais Samia Kwa kunipa nafasi ile pamoja na mazungumzo mazuri yalivyo kwenda Nampa ahsante Kwa kufungua malango la maridhiano"


Alisema Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kuzungumza na yeye na kutaka kutafuta mwafaka wa kisiasa Kwa kuondoa maumivu ya kisiasa nchini na kuweka misingi bora ya Demokrasia nchini .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI