Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea Mwl. Lutta Rucharaba (Omwami) Jumanne March 15, 2022 alifanya ziara ya kwenda kuona maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kifuru kwa Masister, Barabara ya Msome iliyojengwa kwa dharura ili kupata njia mbadala wakati wa ujenzi wa daraja la Kifuru kwa Masister ukiendelea, Barabara ya kwenda kanisa la Roma Mtaa wa Kwa Limbanga (Kata ya Kinyerezi) Maendeleo ya ujenzi wa mfereji wa Maji Bonde la Sungura eneo la Mtaa wa Sokoine na uharibifu unaosababishwa na magari makubwa ya mizigo katika Barabara ya Tasaf (Kata ya Kimanga)
Katika ziara hiyo Katibu wa Mbunge alifuatana na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala Eng .Silvester Chinengo ambaye amemhakikishia Katibu wa mbunge kuwa anafahamu jitihada kubwa za Mhe. Mbunge za kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na changamoto walizo nazo lakini haswa kuhusu daraja la kwa Masister amesema kuwa Mkandarasi M/S Bronze Tech Co. Ltd ambaye ndiye anajenga daraja hilo anatambua umuhimu wa Hilo daraja na hivyo atahakikisha anasimamia anakamilisha kazi ndani ya wakati.
Kufuatia ziara hii, Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Ladislaus Kamoli amemtumia Salaam za shukrani na pongezi Eng. Chinengo kwa kazi kubwa na ya kizalendo anayoifanya katika kuhakikisha miundombinu ya Wilaya ya Ilala inaimarika.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Segerea
0 Comments