Adeladius Makwega-KONGWA.
Machi 23, 2022 nilikwenda wilaya ya Kongwa-mkoani Dodoma ambapo ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya harakati za Ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika.
Wakati zoezi lilipokamilika nilitoka nje ya bwalo kubwa la eneo hili lenye Shule ya Sekondari ya Kongwa na kukutana na watu kadhaa walikuwa wakizungumza, kwa kuwa nilikuwa nasilikilza habari za harakati za ukombozi niliamua kukaa na ndugu zangu hawa angalua kubalishana mawazo.
Nikiwa hapo nilikutana na mandhari ya miti mingi mirefu ambayo inaonekana ni ya miaka mingi hata harakati za ukombozi barani Afrika imeshuhudia.
Kama ningekuwa na nguvu ya kuipa uwezo miti hiyo kusema, leo hii ningewasimulia lakini miti hii imebarikiwa kuwa bubu hata kutamka nukta moja ya neno japokuwa ina uhai.
Eneo hili la kambi ya Wapigania Uhuru wa Kongwa wa zamani lina miti mingi ya asili kuliko ya kupandwa .na jambo hilo lilinipa hamasa ya kutaka kujua jina halisi ya miti hii ya asili.
Ndugu hawa nilipowauliza waliniambia kuwa miti hiyo inaitwa MGUNGA (umoja) MIGUNGA (wingi). Kwa kuutazama ni mti wenye miba tele, majani membamba, madogo madogo .
“Jina hilo Migunga ni jina la kwetu Uheheni, sifahamu Wagogo wanauhitaje.”
Aliniambia ndugu Richard Kivike kutoka Wizara ua Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye nilikuwa naye jirani.
“Miti hiyo inapendwa sana kuliwa na tembo na ndiyo chakula chao kikuu.”
Niliendelea kusikiliza elimu hiyo ya miti ya MIGUNGA chini ya mwalimu wangu Mnyalukolo ndugu Kivike.
Mbona ina miba mingi? haiwezi kumletea madhara tumboni? (Niliuliza)
“Tembo akila hapati madhara yoyote yale, tena inadaiwa kuwa inasaidia hata kama anapatwa na minyoo basi yote inatoka tumboni akijisaidia.”
Mwanakwetu, kumbe jambo linaweza kuwa hatari kwako lakini lina faida kwa mwingine.
Mara tulijulishwa kuwa chakula kipo tayari na nasi kujongea foleni ambayo ilikuwa ndefu kidogo. Niliunga foleni hiyo ambayo kwa nyuma yangu kulikuwa dada mmoja mchaga, dada mwingine Mndamba na jamaa mwingine ambaye sikumfahamu kabila lake na mbele yangu kulikwa na watu wawili ambao walikuwa wamevalia sare za CCM mama na baba (wote walikuwa Wagogo)
Niliwasalimu ndugu hawa kwa salamu ya chama hiki na wao wakanijibu, kidumu.
Niliwauliza swali nyinyi katika CCM ni kina nani?
“Sisi ni wajumbe wa CCM wa Kamati ya siasa ya Wilaya.”
Mjumbe mwanamke alinijibu huku tfoleni ya chakula inasogea.
Nikasema ahaa.
“Mkuu wetu wa wilaya ametuomba tuje kushiriki maana amepata ugeni mkubwa kutoka Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.”
Nikamjibu, hongereni sana.
Na wewe ni nani? Niliulizwa
“Mimi ni mwalimu natokea huko Mlali, niliposikia wageni hawa wanakuja leo nikaamua na mie nije kusikiliza.”
Nilimjibu kwa jibu la utani mama huyu.
Nilimuuliza mbona mjumbe mmoja wa kamati ya siasa simuoni?
“Nani? Mbunge wetu (akajijibu), yupo.”
Basi mjumbe huyu wa kamati ya akawa anawakaribia wagawaji wa chakula.Yeye mbele mimi nyuma,nikamgusa begani huku nikitupia swali lingine
Mara ya mwisho umemuona lini mjumbe mwenzako wa kamati ya siasa?
“Disemba mosi, 2021.” Alijibu.
Nilichukua chakula na mie kula haraharaka na kuwahi kurudi kwangu madongo poromoka.
Nilipotoka hapo nilifurahi mno kwa mambo makubwa matatu, moja kuufahamu mti wa MIGUNGA, pili kuongea na mjumbe huyu wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Kongwa na tatu kufika katika wilaya hii ambayo ndipo nilipozaliwa miaka kadhaa iliyopita ambapo wazazi wangu walikuwa watumishi.
Nikasema niwasimulie furaha yangu mara tatu nikiwa KONGWA.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
0 Comments