Header Ads Widget

EAC YASAIDIA TANZANIA ....

Mkurugenzi wa idara ya utalii,Philip Chitaunga

serikali nchini Tanzania kwa kushirikiana sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki inatoa mafunzo  ya upangaji wa madaraja na upimaji wa ubora wa huduma za malazi na chakula ili kuongeza idadi ya wataalamu hao nchini katika sekta ya utalii. Mwandishi Teddy Kilanga,MDTV Arusha 

Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya upangaji wa madaraja na upimaji ubora wa huduma za malazi na chakula katika chuo cha Taifa cha utalii Arusha,Mkurugenzi wa idara ya utalii wa wizara ya maliasili na utalii,Philip Chitaunga alisema mafunzo hayo mahususi yatakwenda kuongeza idadi ya wataalamu katika sekta hiyo.

"Wanaopewa mafunzo haya ni wanafunzi 44 ikiwa lengo letu nikuongeza kasi ya kupanga huduma za malazi katika madaraja ubora nakusaidia kutambulika nje ya nchi,"alisema Mkurugenzi huyo.

Afisa Mkurugenzi mtendaji mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii,Dkt.Shogo Sedoyeka

Alisema umuhimu wa mafunzo hayo ni pamoja na kujenga wataalamu wa ndani katika nchi yetu ili baadaye watumike katika kupanga huduma za malazi,chakula katika daraja na upimaji ubora lakini vigezo vinavyitumika kwenye kupanga huduma hizo ni kutoka katika sekretarieti ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha alisema mshiriki atakayehitimu mafunzo hayo kupanga huduma za  malazi kwa nchi yeyote hivyo serikali imeamua kufanya mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani ya nchi kupitia sekta hiyo.

Aliongeza kuwa sasa hivi wizara ya maliasili na utalii inaunda mfumo wa kieletroniki ambao utatumika kurahisisha kupanga zoezi hilo la upangaji wa malazi katika madaraja yenye ubora hivyo wadau wataanza kujitathmini wao wenyewe.

Chitaunga alisema wameamua kutumia sekta binafsi ili kujenga uwazi wa mafunzo hayo kwani wao pia wanahusika katika utoaji huduma muhimu za malazi n madaraja yenye ubora pia inajenga umoja kati ya serikali na sekta binafsi kwa lengo la kuwezesha biashara iweze kufanyika.

Kwa upande wake Afisa Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii,Dkt.Shogo Sedoyeka amesema hadi sasa wameshamaliza mafunzo ya awamu ya kwanza ya kuwaongezea ujuzi wadau muhimu katika mnyororo wa utalii kutoka mikoa 8 ya Tanzania bara ikiwemo mkoa wa Lindi,Mtwara na  Ruvuma.

"Mikoa mingine ni Njombe,Iringa,Mbeya,Mara na Mwanza ikiwa mafunzo hayo yalitolewa kwa washiriki 100 hadi 150 kwa kila mkoa ikiwa hadi sasa wametoa mafunzo kwa washiriki wapatao 1200,"alisema Dkt.Sedoyeka.

Dkt.Sedoyeka alisema mafunzo ya awamu ya pili ni upangaji wa madaraja na upimaji wa ubora wa huduma za malazi na chakula ambayo yanatolewa katika chuo cha Taifa cha utalii tawi la Arusha ambapo itakuwa na washiriki 44 kati ya hao 14 ni kutoka sekta binafsi na 30 kutoka sekta za umma.

"Watoa mafunzo wakuu ni wale wanaotambulika na jumuiya ya Afrika ya mashariki ambapo kwa Tanzania waliopo ni wachache sana ukilinganisha na ukuaji wa sekta ya utalii nchini na hali hii kupelekea kuwa na umuhimu sana,"alisema Dkt Sedoyeka.

Naye Afisa elimu sekondari mkoa wa Arusha Abel Ntupwa alisema kama wadau wa utalii ni vyema washiriki hao wa mafunzo hayo wakawajibika ili kuongeza utalii nchini Tanzania pamoja  na  kuiletea heshimaTaifa lao.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Rauliano Munishi alisema ni vyema mafunzo hayo yakawa ya vitendo kutokana na baadhi ya watanzania kutokuwa na uzoefu wa kazi.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI