Header Ads Widget

BREAKING NEWS: OFISI ZA MANGE KIMAMBI APP ZAVAMIWA, WAKAMATA WAFANYAKAZI NA VIFAA

Na Mwandishi wetu, Matukio Daima blog Dar

Vyombo vya Usalama  vimevamia ofisi za mtandao wa Mange kimambi wa Mange Kimambi App zilizopp Kinondoni Mtaa wa Togo na kuwakamata Wafanyakazi wote pamoja na kuondoka na vifaa vya ofisi hiyo.


Tukio hilo limetokea majira ya jioni ya Machi 14/2022 ambapo Vyombo hivyo vya Usalama wakiwa kwenye magari zaidi ya Manne ikiwemo Noah, Land Cruiser  mbili ambapo walizingira jengo hilo la gorofa 4 na kisha kuwavamia katika ofisi hiyo ya Mange ilipo gorofa ya 3 na kuwakamata wafanyakazi hao.

Hata hivyo hadi sasa bado taarifa rasmi kutoka kwa jeshi hilo hazijaelezea lolote wala kutolea ufafanuzi juu ya kuwashikiria.

"Wawili wapo kituo kikubwa cha Polisi pale Central Dar es Salaam.

Tunaendelea kufuatilia kufahamu zaidi" kilieleza chanjo cha taarifa.

Juhudi za kuwasiliana na jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam zinaendelea baada ya awali simu yake kutokuwa hewani




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI