Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la JPM (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa kilometa 3.2 na linalokatiza katikati ya Ziwa Victoria.
Mradi huo unaoghalimu Sh716.33 bilioni umefikia asilimia 40.2 huku ukitarajiwa kukamilika Februari 24, 2024.
Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Kasekenya ameiagiza Tanroads kusimamia ujenzi huo ili kuhakikisha unakamilika ndani ya wakati uliopangwa.





0 Comments