Header Ads Widget

SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZAPELEKEA KUKOSEKANA KWA MAJI

 



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amesema  kuwa hapa nchini na duniani kote maji yamekuwa yakipungua kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo kilimo na ukataji miti holela karibu na vyanzo vya maji.


Ameyabainisha hayo katika kikao Cha kwanza Cha jukwaa la wadau wa Usimamizi wa raslimali za maji katika kidakio Cha Kikuletwa kilichofanyika Mkoani Kilimanjaro.



Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyanzo vya maji ni sehemu ya Mazingira ya Binadamu hivyo Kila mmoja anajukumu la kulinda na kuhifadhi raslimali za maji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na Wananchi.



Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la Mto Pangani Segule Segule amesema agizo ambalo limetolewa na mkuu wa mkoa amelipokea na litafanyiwa kazi Kwani tayari wameweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza alama za Mipaka katika maeneo tengefu ya vyanzo vya maji na kuwashirikisha wadau wa Usimamizi wa raslimali hiyo.



 Kwa upande wao  washiriki katika kikao hicho akiwemo  profesa Aidan Msafiri amesema tatizo la uharibifu wa Mazingira ni la kimaadili huku akiwataka wadau wengine walioshiriki kikao hicho kulichukulia suala la utunzaji wa Mazingira Kwa wigo Mpana.


Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrick Boisafi ametaka mipango kuimarishwa ili jamii ivune maji ya mvua kwa ajili ya kukabiliana pale penye upungufu.


Amesema ni jukumu la wadau kwa pamoja kuhakikisha maji yanayovunwa yanatumika kwa ajili ya umwagiliaji, mifugo na matumizi mengine yatakayoepusha migogoro hususani ya wakulima na wafugaji.


Hata hivyo Afisa mazingira wa PBWB, Eng. Arafa Majidi ametoa wito kwa taasisi za umma kuwa na mipango ya pamoja katika matumizi bora ya ardhi kwani yanahusisha matumizi ya maji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI