Header Ads Widget

SHIRIKA LA (CIT) LASAIDIA KUPATIKANA KWA ZAIDI YA SH.MILIONI 700 KWA AJILI YA KUSAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI.

 




ARUSHA



Zaidi ya Tsh.milioni 700 zimepatikana kutoka kwa wananchi wa nchi ya Uswisi kwa lengo la kusaidia watoto wenye uhitaji walioko nchini Tanzania pamoja na kuendesha huduma ya mama na mtoto.



Akizungumza katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro, Mkurugenzi wa shirika la kikristo la kimataifa linalojikita katika maendeleo na utetezi wa mtoto (CIT) Mary Lema alisema zoezi hilo wameliandaa kwa kushirikiana na  shirika la compassion  International  Switzerland pamoja na Muskathlon Switzerland kwa lengo la kuwasaidia watoto wahitaji.



Mkurugenzi huyo alisema wananchi hao wa nchi ya Uswisi wamefika nchini Tanzania kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni kilele cha kuchangisha fedha za kuwasaidia watoto wehitaji wa nchi ya Tanzania ambapo wameshaanza safari ya kupanda mlima huo.



"Lakini Muskathlon ni mjumuiko wa watu mbalimbali wenye maono ya kutetea haki za wanaoonewa,kujijenga kiimani na kiafya kwa kufanya  shughuli zitakazo hitaji nguvu na kujitoa kwa ajili ya wengine ambapo ilianza na watu wanne na sasa inawanachama maelfu,"alisema Mkurugenzi huyo.




Aidha Lema alisema kuwa kupitia ushirikiano huo wameshachangisha  fedha zaidi ya sh.milioni 700 ikiwa ni zaidi ya lengo ambapo zitatumika katika kuendesha huduma ya mama na Mtoto pamoja na kufadhili watoto wanaotoka familia zenye uhitaji hapa nchini.

Lema alieleza kuwa tangu kuanza kwa uchangishaji huo wa fedha takribani miaka sita iliyopita wamefanikiwa kupatikana zaidi ya sh.bilioni 9.7 na kutumika katika kufadhili miradi mbalimbali hapa nchini na nchi nyingine zenye huduma za compassion.



"Wageni zaidi ya 300 wameingia nchini katika kipindi hicho kutoka Uholanzo,Ubelgiji,Ujerumani na Uswisi hivyo kuchangia pato la Taifa kupitia utalii ambapo wageni hao 26 mbali na kuwepo nchini kwa lengo la kuchangisha fedha wamekutana na watoto wanaowafadhiri na kutembelea  vituo kadhaa ambavyo vinaushirikiano na shirika la Compassion International Tanzania,"alisema.



Alisema wananchi hao wa Uswisi watakuwepo nchini kwa muda wa siku kumi ambapo watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana hapa nchini.



Pia alisema CIT hutumia mbinu mtambuka katika kukabiliana  na changamoto za maendeleo zinazowakabili watoto masikini katika jamii kwa lengo la kuwakomboa watoto walio katika hali ya umasikini.



Nao baadhi ya wageni hao kutoka nchi ya Uswisi,Christian Willi na Manuela Denoth walisema wamefurahia kupanda mlima huo pamoja na kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji chini ya ufadhiri wa shirika hilo la Compassion.



Mhifadhi wa shirika la uhifadhi Tanzania(Tanapa) katika geti la Machame,David Gordon alisema anashukuru shirika la Compassion kwa kuwaleta wageni nchini kutalii kwani kupitia njia hiyo inachangia  mapatao kwa Taifa hivyo ni vyema mashirika mengine yakaiga mfano huo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI