Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limebadilisha jina ambapo kuanzia sasa litajulikana kama Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Adolf Rutayuga amesema kuwa mabadiliko hayo yamefanywa kwa mujibu wa sheria .
"Kufuatia sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali za Bunge Namba 4 ya mwaka 2021 iliyorekebisha sheria ya baraza, sura 129, tunapenda kuutarifu umma kwamba baraza la Taifa la Elimu ya ufundi NACTE limebadilisha jina na sasa itajulikana kama (NACTVET)"amesema Dkt, Rutayuga.
Amesema kuwa, mabadiliko hayo madogo yameliongezea baraza jukumu la urekebu na udhibiti ubora wa mafunzo ya ufundi stadi ambayo awali yalikua yalikua yakifanyika chini ya mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA).
Ameongeza kuwa, shabaha ya ni kuongeza ufanisi katika usimamizi, urekebu na uthibiti ubora wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa nchini Tanzania.
Hata hivyo, amesema kutokana na mabadiliko ya sheria hiyo, jukumu la urekebu na udhibiti ubora wa mafunzo ya ufundi stadi yamehamishiwa rasmi kutoka VETA na kupelekwa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.
Aidha, amewataka wananchi kuwa maombi yote ya usajili wa vyuo /vituo vya mafunzo ya ufundi stadi yawasilishwe NACTVET ambapo majukumu hayo yamehamishiwa.
Hata hivyo, baraza hilo limetoa wito kwa vituo/ vyuo vyote vilivosajiliwa kutoa mafunzo ya ufundi stadi kuendelea kuendesha mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni zilizopo.
"Baraza litaendelea kushirikiana na wadau wote, ikiwa ni pamoja na vyuo katika kuendeleza kukuza utoaji wa elimu bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu" amesema Dkt Rutayuga.





0 Comments