Na Amon Mtega,_Songea.
MKUU wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Pololet Mgema amekiomba Chuo Cha Taifa cha Utalii kuanzisha tawi la chuo hicho Mkoani Ruvuma ili kutoa fursa ya wengi wa Utalii wapate kujifunza namna ya kuwahudumia wageni(Watalii)kutoka na Mkoa huo kuwa na vivutio vingi.
Ombi hilo amelitoa wakati akifunga mafunzo ya Uviko19 kwa wadau wa utalii wa Mkoani humo namna ya kujikinga na kuwakinga wageni pindi wanapo talii kwenye vivutio mbalimbali vya Mkoani huo .
Mgema akifunga mafunzo hayo kwa washiriki zaidi ya 120 amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma unavivutio vingi hivyo kama kutawekwa tawi la Chuo hicho basi kutatoa fursa kwa wadau wengi kujifunza pamoja na kuibua vivutio ambavyo vimesahaulika ili mwisho wa siku viendelee kuwa na tija kwa Taifa katika suala zima la kuinua mapato.
Mkuu huyo katika hatua nyingine amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo na mapambano dhidi Uviko 19 .
Aidha amempongeza Mbunge wa Jimbo la Songea mjini Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kazi ya kuimarisha sekta hiyo kwa kutengeneza miundombinu bora ya Watalii.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Fedha mipango utawala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (CPA) Munguabella Kakulima awali amesema kuwa mafunzo hayo yataenda kuboresha sekta ya Utalii na kuwa wamejipanga vema kutoa mafunzo hayo.
Kakulima amesema kuwa mafunzo hayo yamefadhiliwa na mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na makabiliano dhidi ya Uviko 19 katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo yanafanyika katika mikoa nane hapa Nchini .
Naye mmoja wa washiriki Rukia Ismaily ambaye ni mfugaji Nyuki katika Wilaya ya Songea amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia hasa pindi wageni wanapohitaji huduma ,huku akiunga mkono hoja ya kuwepo kwa tawi la Chuo cha Taifa cha Utalii Mkoani humo.
Hata hivyo mmoja wa wahudumu wa Hotel Eunike Haule amesema kuwa kufuatia mafunzo hayo yatamsaidia kuwatambua wageni nini wanahitaji kuhudumiwa tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya kupatiwa mafunzo hayo.
0 Comments