Na Hamida Ramadhan Dodoma
MKURUGENZI Wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amewaongoza wakazi wa Kata ya Changombe Jijini hapa kufanya usafi,huku akidai wameanza zoezi la usafi wa kata kwa kata lengo likiwa ni kuhakikisha Jiji hili linakuwa safi.
Hayo amesema leo jijini hapa wakati wa zoezi la ufanyaji wa usafi pamoja na upandaji wa miti katika Kata ya Chan'gombe ambapo amesema wanafanya vitu viwili kwa wakati mmoja ambavyo ni usafi wa mazingira na kupanda miti na wamesha tembea katika kata sita za jiji la Dodoma .
Amesema sheria za mazingira zipo na wananchi wengi hawazifahamu kwa wale wanaozifahamu wamekuwa hawazizingatii lakini sheria zipo na zinabana faini kubwa kwani ni kuanzia 50000 hadi 300000.
" Hapa tumewasikia wananchi wa kata ya Changombe Pampas mtu anatoka nyumbani kwake anakuja kutupa mfuko wa Pampas katika eneo la shule sasa tunafanya vitu viwili tunaotoa elimu na tunatekeleza sheria ya mazingira na ndio maana tunaongozana na polisi jamii pale tutakapo mkuta mtu anachafua mazingira hapo hapo anachukuliwa hatua" amesema Mafuru.
Sambamba na hilo amesema wamesambaza miti kwenye shule zote miti Milioni 1.5 wameshasambaza kama Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira amesema Seleman Jafo anavyohamasisha watoto kusimamia miti yao.
" Hivi karibuni jiji la Dodoma Wakala wa Barabara vivijini (TRURA) na Wakala wa Barbara nchini (TANROADS ) tulikuwa na kikaoa na sasa tunakwenda kupanda miti katika Barabara zetu mpya na tutahakikisha ndani ya miezi mitatu mbele kila mtu atakuwa na muamuko wa kufanya usafi kuanzia chumbani kwake mpaka nje.
Kwa upande wake,Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma,Dickson Kimaro amesema wamekuwa wakiendelea na zoezi la utoaji wa elimu kuhusu uzoaji wa taka ambapo kaya nyongi zimekuwa zikunitokeza kufanya usafi.
Amesema Kupitia mgambo wa jiji la Dodoma watawakamata na kuwatoza faini ya shilingi 50000 hadi 300000 wale wote watako fanya uchafuzi wa mazingira ambapo amesema nusu ya fedha itarudi kwa aliyetoa taarifa kwa mtu aliyefanya uchafuzi wa Mazingira .
0 Comments