Header Ads Widget

"WANAUME KAPIMENI SARATANI YA TEZI DUME KUNA VIPIMO VIPYA NA VYA KISASA" UMMY MWALIMU

 



Na Hamida Ramadhan Dodoma 

 


WAZIRI wa Afya Ummy mwalimu amewataka wanaume kuacha kuogopa kupima Saratani ya Tezi Dume kwani  kuna vipimo vipya na vya kisasa tofauti na ile njia ya upimaji wa zamani .


Hayo  ameyasema jijini Dodoma wakati  akitoa tamko  katika maadhimisho ya siku ya saratani Duniani kwa mwaka 2022 yenye kauli mbiu isemayo  "Huduma za saratani sawa kwa wote


Vipimo vitakuwepo katika vituo vyote kuanzia ngazi za kutolea huduma za afya ambapo amesema pia wanaume wamekuwa wakikabiliwa na saratani ya Tezi dume asimilia 21 saratani ya  Koo kwa asilimia 11.8 Kinywa na mdomo kwa asimia 7.3 Utumbo mdogo asilimia kwa asilimia  9 na mkubwa. 


Amesema kwa upande wa wanawake saratani inayowaathili zaidi ni saratani ya kizazi kwa asilimia 43 saratani ya matiti 14.2  na Saratani ya koo  kwa asilimia 3 .8


"Na ndio maana nasema kama tukifanikiwa kupunguza saratani ya Mlango ya kizazi maana yake tutapunguza wagonjwa wa saratani kwa asilimia 40," Amesema  


Na kuongeza kuwa "Ugonjwa wa saratani na magonjwa mengine yasio ambukiza yanachangiwa na mtindo wa maisha kama vile ulaji mbaya, kutokufanya mazoezi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI