Mkuu wa wilaya Ulanga mkoani Morogoro Ngollo Malenya amewataka watumishi wa afya kuzingatia weledi na kanuni za utumishi wao ili kundoa Changamoto mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo .
Malenya ameyasema hayo wakati alipotembelea hospitali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kutembelea wagonjwa kuwapa zawada za sikukuu na kuona utendaji kazi watumishi wa hospitali hiyo
Amesema watumishi wa afya wananafasi Kubwa ya kuwapa faraja wagonjwa hivyo wanapaswa kutumia lugha za stara Kama sheria za utumishi zinavyotaka.
Katika zoezi Hilo Dc Malenya amegawa msaada was vitu mbalimbali ikiwemo parcel yenye Matunda, maji, juice, dawa za mswaki, sabuni ya Unga, sabuni ya mche na fedha Kama ishara ya upendo
"nimeona nifike hapa hospitali ili kuwapatia zawadi ya vitu mbambali ili ziweze kuwasaidia lakini Ni wajibu wetu Kama viongozi kutembelea wananchi wetu kujua huduma wanazopata katika taasisi za serikali" Ngollo Malenya DC Ulanga
Katika hatua nyingine Dc Malenya amezindua zoezi la upandaji miti na kusisitiza utunzaji wa mazingira ambapo amesema zoezi Hilo litakua endelevu





0 Comments