WAKAZI wa Kijiji cha Mtumbatimaji kata ya Mgombasi wanaofanya shughuli za kibinadamu(Kilimo) katika eneo la Kihindambue wameanza kutolewa katika eneo hilo kwa lengo la kupisha uhifadhi uliyopo katika mlima wa Linole hifadhi ya milima Matogoro ‘B’huku wakazi hao wameiomba Serikali iwaachie waendelee kufanya shughuli za kibinadamu...........NA AMON MTEGA,NAMTUMBO.
Wakizungumza wakazi hao kwa nyakati tofauti mkazi Twaliki Mbilo amesema kuwa eneo hilo walipewa na Serikali ya Kijiji cha Mtumbatimaji tangu mwaka 2014 na kuwa katika kipindi hiki cha karibuni wakaona wanaambiwa wahame katika eneo hilo kuwa ni Hifadhi ya maliasili jambo ambalo linadaiwa linashangaza wakazi huo .
Mbilo amesema kuwa wanahamishwa kwa nguvu na kuwa yeye ameezuliwa nyumba huku mahindi aliyokuwa ameyahifadhi ndani amedai kuwa yamebebwa pamoja na kuku zilizokuwemo kwenye banda hivyo wanaiomba Serikali ingewaachia eneo hilo kwa madai kuwa ndiyo sehemu wanayojipatia ridhiki .
Mkazi mwingine Athumani Mapunda ambaye inadaiwa nyumba yake imechomwa moto na mbuzi 16 wamechukuliwa amesema kuwa majira ya mchana aliwaona watu wameenda katika nyumba hiyo na waichoma moto yeye alikimbia huku mbuzi wanaodaiwa walikuwa bandani walichukuliwa.
Kufuatia sakata hilo mwenyekiti wa Kijiji cha Mtumbatimaji Liwanda Makunjalila amesema kuwa mikutano ya makubaliano ya kuwahamisha wanaofanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo ilifanyika na walifikia makubaliano mbele ya mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dr.Julius Ningu.
Mwenyekiti huyo amesema kufuatia mkutano huo uliofanyika chini ya mkuu wa Wilaya huyo yalifikia makubaliano ya kuwatambua wakazi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika eneo hilo ambapo ofisi ya kijiji ilifanya na taarifa hizo zimepelekwa katika ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Kwa upande Mkuu wa Wilaya hiyo Dr.Julius Ningu amesema kuwa eneo hilo la milima wa Linole ni hifadhi ya Milima Matogoro ‘B’ hivyo makubaliano wananchi wanatakiwa kuliachia ili shughuli za uhifadhi ziendelee wa misitu na vyanzo vya maji vifanyike .
Dr.Ningu amesema kuwa kabla ya makubaliano hayo mkutano ulikaliwa na ofisi yake iliagiza kwenye ofisi ya kijiji kwenda kuwaorodhesha watu wote waliopo kwenye eneo hilo ili kupata takwimu sahihi.
Mkuu wa Wilaya hiyo kuhusu baadhi ya watu ambao wanadaiwa kuezuliwa Nyumba na kuchomewa amesema hilo halijui kwa kuwa hakuna nyumba inayojengwa ndani ya hifadhi.





0 Comments