Madereva na wamiliki wa magari wametakiwa kuacha tabia ya kupatana (kubagein) na watu wanaosimamia maegesho ya magari jijini Dar es Salaam kwani haiwasaidii kukwepa kulipa tozo za ushuru wa magari........Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam Eng Geofrey Mkinga wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesema watu wengi wamekua wakipatana na wasimamizi hao Ili kukwepa kulipa ushuru wa maegesho ya magari.
Amesema kuwa, tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo kilichobainika kuwa fedha nyingi zipo mikononi mwa watu kutokana na kulimbikiza madeni na kukwepa kulipa ushuru.
"Naomba tuache tabia ya kubagein na hawa wasimamizi wetu kwani haisaidii chochote, mnaweza mukapatana lakini kupitia mfumo huu utafanyiwa uhakiki ikibainika gari lako halijafanyiwa scan ukaingizwa kwenye system utalipa madeni yote"amesema Eng Mkinga.
Aidha amewataka watu kulipa ushuru wa maegesho ya magari kama sheria inavyoelekeza ambapo siku moja ni shill 2500, na saa moja sh 500 na endapo itapita siku 14 bila kulipia madeni utapigwa faini ya shill 10000.
Hata hivyo, amewataka watu wasajili vyombo vyao Ili waweze kupata namba halisi ya mmiliki wa chombo ambapo itamsaidia mmiliki huyo kupata taarifa zote zinazohusika na masuala ya ushuru wa magari kwenye maegesho.
"Tutakapoanza kutekeleza sheria watu watalazimika kulipa, baada ya siku 14 kupitia faini itakua sh 10000, naomba watu wajisajili Ili Ili tupate namba halisi ya mmiliki wa chombo apate faida mara mbili ikiwemo kupata kupata taarifa zake "amesema Eng Mkinga.





0 Comments