Header Ads Widget

WANANCHI ONDOENI HOFU MAHINDI YAPO YA KUTOSHA -CPB


BODI ya  nafaka na mazao  mchanganyiko (CPB) kanda ya  nyanda  za  juu  kusini  imesema  kuwa  pamoja na  zoezi  linaloendelea na  uuzaji  wa mahindi nje ya  nchi   ila bado  hifadhi ya mahindi katika  vituo  vyake  ni  kubwa zaidi   na  bei ya mahindi haijapanda   sana  ukilinganisha na mwaka 2016.

Kuwa  mwaka  2016  bei ya mahindi   mwezi kama  huu Januari  ilifikia hadi  shilingi 1050  ila  kwa mwaka huu  bei ya mahindi  kwa  kilo  ni kati ya  shilingi 500 hadi 600  kwa  kilo  moja  hivyo  hali ya  chakula  bado  ni  nzuri  na haitegemewi  kuwa  mbaya maana  akiba  ya mahindi  waliyonayo ni  kubwa  .

Akizungumza  Leo na Matukio Daima Media kwa  niaba ya meneja  wa Bodi ya nafaka  na mazao  mchanganyiko   kanda ya  nyanda za  juu  kusini    Anganyila Kamihanda   alisema  kuwa  lengo kubwa la  taasisi  hiyo ni  kuendelea  kufanya  biashara  na  sasa  biashara kubwa ni  uuzaji  wa zao la mahindi ambalo  siku  za  nyuma  hali  ya  uuzaji  wa mahindi  ilikuwa  mbaya  zaidi kabla ya  serikali  kuruhusu  mazao  kuuzwa  nje ya  nchi .

“ Ikumbukwe hapa  kati kati  hali ya uuzaji  wa mahindi  ilikuwa  mbaya  hadi kupelekea  hifadhi  zetu  kujaa ila  sasa  tumefanikiwa  kupunguza  akiba  kubwa ya  mahindi  tuliyokuwa nayo kwa  kupitia  mikataba   ya  ununuzi  wa mahindi  tuliyoingia na kampuni  za  Rwanda na  Kenya “ alisema

Alisema  katika  kituo  cha  Iringa  walikuwa na hifadhi ya  mahindi  ambapo  walikuwa na tani 18,000  za mahindi   kabla ya  Rwanda  kununua  tani  5000  hivyo  akiba  ambayo  watabaki nayo ni  tani  13000   za mahindi  ambayo  wanaendelea  kusaga unga na kusambaza  ndani ya  nchi kwa gharama  nafuu  zaidi .

Pia  alisema  kwenye  vituo  vingine  vya Songwe na  Songea mkoa  wa Ruvuma  bado  wanayo hifadhi  ya kutosha  ya  mahindi na kama  hali ya ukame  itaendelea  bado  hakutakuwa na  hofu   yoyote maana  hifadhi ya  mahindi  iliyopo  ni  kubwa  zaidi  kwao na pia  hifadhi ya  Taifa  ya  chakula wana akiba ya  kutosha  ya mahindi .

Alisema  kuwa  ikitokea  mahindi  yamepungua watakwenda  kuchukua  mahindi kwenye  hifadhi ya  Taifa ya nafaka  ambako  kuna  akiba ya  kutosha ya mahindi .

Alisema  kuwa  kwa   kawaida  bei ya  mahindi  iliyopo  ni  nzuri  sana na nafuu kwa  wananchi kwani  kama  bei ya  mahindi  ingepanda mwezi  wa 9 ama wa 10  ndipo  huwa mbaya  zaidi  ingefikia  bei  hiyo kwa  miezi tajwa  basi  hofu  ingekuwa  kubwa  zaidi lakini pamoja na changamoto  za  mvua zilizokuwepo  bei ya mahindi  haitapanda   badala  yake  mwakani wakulima  watakuwa na neema  zaidi ya bei  nzuri ya mazao .






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI