Wananchi wa Kitongoji Cha Kikonga kijiji Cha Kisanga Wilaya Kilosa Mkoa wa Morogoro wameanza ujenzi wa zahanati ambayo itasaidia kutoa huduma kwa watu zaidi ya elfu tatu
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Christopher Petro amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekuja baada ya wananchi kupata changamoto ya kupata huduma ya afya kwa kutembea zaidi ya kilometa 15 Hadi katika Zahanati ya kijijj na kusababisha baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia njiani
Petro anasema baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo wamekubaliana wananchi kuchangia fedha kiasi Cha shilingi elfu tano kwa kila mwananchi.
"kila mwananchi amechangia elfu tano ambapo Hadi Sasa tumepata zaidi ya milioni mbili hivyo tuneoba tuanze na msingi huku michango inaendelea" Chistopher Petro mwenyekiti kitongoji Cha Kikonga
Naye Amina Seleman mkazi wa Kijiji hicho anasema licha ya Zahanati hiyo kuwa mbali bado huduma zinazotolewa haziridhishi hivyo kukamilika kwa ujezi wa Zahanati hiyo utaokoa vifo vya watoto na wajawazito
Katika kuunga mkono juhudi za wananchi Viongozi mbalimbali wameahidi kuchangia ambapo Mkuu wa wilaya ya Kilosa Alhaj Majd Mwanga ameahidi mifuko ya saruji 64
DC Mwanga anasema lengo la serikali ya awamu ya nne kuhakikisha wananchi wanapata huduma Bora za afya hivyo watahakikisha Zahanati hiyo inakamilika kwa wakati hivyo ataendela kuchangia Mara kwa mara
Wengine waliotoa ahadi za michango ni pamoja na chama Cha Mapinduzi wilaya ya Kilosa kimeahidi kutoa Bati mia mbili na mbunge wa Jimbo la Mikumi Denis Londo akiahidi mifuko 150 ya Saruji.
Dokta George Kasibante NI Mganga mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa anasema tayari serikali imeanza mchanakati wa usajili wa Zahanati hiyo
Dokta Kasibante anasema wananchi wengi wamekua wakijenga vituo vya afya na Zahanati bila kushirikisha uongozi jambo linasababisha ucheleweshaji wa usajili
Zaidi ya asilimia tisini ya ujenzi wa Zahanati hiyo utatumia nguvu kazi za wananchi huku malengo ya serikali kila Kijiji kuwa na Zahanati ambapo Kijiji hicho kitakua ja Zahanati mbili .





0 Comments