Wakulima wanaolima mazao kilimo hai nchini (Kilimo Ekolojia) wameiomba Wizara ya kilimo kulifanyia kazi agizo lililoaihidiwa na aliyekuwa naibu waziri wa kilimo ambaye kwa sasa ni waziri wa Wizara hiyo Husseni Bashe la kuanziasha benki ya mbegu za asili Nchi ili kuongeza mahitaji ya mbegu hizo kwa wakulima..............Na Rehema Abraham
Katika mkutano wadau wa kilimo hai uliofanyika Jijini dodoma September mwaka jana 2021 waziri bashe alisema kwamba Wizara itahakikisha kwamba itaanzisha kitengo maalum kitakachokuwa kinahusika na mbegu za asili ili kutunza na kuzihifadhi zisiendeelee kupotea.
Akiwa katika mafunzo na wakulima wa kilimo hai walipo katika mtandao wa slow food Tanzania Network kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro mratibu wa mafunzo hayo Frenki Ademba kutoka katika mtandao huo amesema kuwa ni vyema agizo hilo likafanyiwa kazi ili kunusuru mbegu za asili ambazo zimekuwa katika hatari ya kupotea.
Sambamba na hayo amesema kuwa mtandao huo una mpango mkakati wa kuanzisha bustani za asili katika shule mbalimbali ili kuwarithisha watoto na kifundishia umuhimu wa kilimo hai kuanzia wakiwa wadogo.
Mratibu wa slow food International Reguli Marandu amesema kuwa pindi mkulima anapotumia mbolea za viwandani ardhi inapoteza uwezo wake wa kustahimili na kuyototoa rutuba nzuri kwa ajili ya kuzalishia mimea.
"Kwa hiyo basi unapozidi kutumia mbolea za viwandani ,sio kwamba unapunguza wadudu Bali wanaongezeka hivyo kuhitaji mbolea zaidi za viwandani"Alisema.
Amesema kuwa dhana ya slows food Tanzania Network itatufanya tujitathmini na kuangalia nyuma tulipotoka kwani vyakula vya asili vinapotea na utambulisho wa vyakula hivyo pia vinapotea.
"Kwa mfano ukienda rombo Kuna aina ngapi za ndizi zilizopo kwenye mashamba Kuna aina zaidi ya 5 na sio 10 Kama ilivyo kwa kipindi Cha nyuma ,lakini pia tumepoteza kitu kinachoitwa biodiversity ambayo ni kilimo mchanganyiko Cha mimea na na wanyama ambayo ilikuwa hapo nyuma"Alisema Marandu.
Hata hivyo Amesema kuwa Kuna Baadhi ya mazao yaliyokuwepo hapo nyuma ambayo kwa sasa yameanza kupotea na mfano wa mazao hayo ni pamoja na ndizi kitarasa ambayo ilikuwa ikipandwa kwa wingi mkoa wa Kilimanjaro lakini kwa sasa mashambani imekuwa chache.
Hata hivyo baadhi ya wakulima walioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo bi Neema Mwendo amesema kuwa ni vyema wazazi wakawarithisha watoto wao ulaji wa vyakula vya asili ili wanapokuwa waelewe umuhimu wa vyakula hivyo .
"Mtoto anatoka shule unampa ngararimu hataki hata wakati mwingine hataki chai na viazi anasema viazi vina viungulia ,Yaani kitu kikubwa tunapolima tuwarithisheshe watoto toka wakiwa wadogo " Alisema.





0 Comments