Viongozi mbalimbali mkoani Kagera wamekutana na kupendekeza zaidi ya shilingi bil.346 zitolewe kwaajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.Na, Titus Mwombeki-MDTV BUKOBA.
Hayo yamesemwa na katibu tawala msaidizi mkoani kagera Nesphori Bwana Katika kikao cha kamati ya ushauri kilichofanyika katika manispaa ya Bukoba wakati akiwasilisha mapendekezo na mipango mkakati iliyopangwa kutekeleza mkoani Kagera kwa mwaka fedha2022/2023.
“Tunamshukuru Mungu mapendekezo yamepokelewa vyema na yamepitishwa kwaajili ya kupelekwa serikalini kwa hatua nyingine, fedha hizi zilizoombwa nikwaajiri ya maendeleo kwa mkoa mzima kwa maana ya sekretalieti ya mkoa pamoja na wilaya zake zote(8) na zitajumuhisha mishahara , matumizi mengineyo pamoja na miradi ya Maendeleo”.
Aidha ameongeza kuwa mkoa wa Kagera unavyanzo mbalimbali vya ndani ambavyo uchangia na vitachangia pia katika bajeti hiyo ili kuweza kusaidia mkoa huo kufikia malengo lengwa.
“Ukiangalia mkoa wa Kagera sehemu kubwa makusanyo tunayo kusanya kwenye vyanzo vya ndani tunavyokusanya kutoka kwenye halmashauri ni kutokana na zao la kahawa, ziwa victoria pamoja na kilimo na ufugaji, hivi vitu vimekuwa vikichangia sana katika kupata mapato kama mkoa na nchi yetu kwa ujumla”.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika kikao hicho Prf.Faustine Kamzora ambaye pia ni katibu tawala mkoa kagera akimuwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Charles Mbuge amewashukuru viongozi walioshiriki katika kujadili na kupitisha mapendekezo hayo na kuwaomba viongozi hao kushirikiana ili kuakikisha mkoa huo unapiga hatua za kimaendeleo.
“ Mkoa wetu unahitaji kipiga hatua kimaendeleo hivyo tushirikiane kama viongozi na tujitoe kufanya kazi ilikufanikisha haya tuliyokusudia”.





0 Comments