Na Mwandishi Wetu, Karatu.
Timu ya Mpira wa Soka ya Wanawake Tanzania, (Tanzanite under20), imewasili katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kutembelea Vivutio vilivyopo katika Hifadhi hiyo.
Timu hiyo ambayo imeweka Kambi Wilayani Karatu Mkoani Arusha ipo katika maandalizi ya kwenda Nchini Ethiopia tarehe 1 Februari 2022 kwa ajili ya kushiriki mchezo wa marudiano na Ethiopia ili kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20.
Timu hiyo umepiga kambi Wilayani Karatu kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ambayo inashabihiana na Addis Ababa Nchini Ethiopia .
0 Comments