Header Ads Widget

TANAPA YAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA VYUO VIKUU NCHINI




NA PAUL WILLIUM, 


Shirika la Hifadhi za Taifa  Tanzania (TANAPA) kupitia Kanda ya Magharibi leo  limefanya  Kongamano la Wanazuoni wa Vyuo Vikuu na Kati vilivyopo ndani ya Mkoa wa Mwanza.



 Kongamano hili lililenga kuhamasisha Viongozi wa Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuanza kushiriki kikamilifu katika uhamasishaji wa Utalii wa ndani katika Jamii zilizopo katika Vyuo Vikuu nchini.


Aidha, Kongamano hilo lililokuwa na Kauli Mbiu ya 'Ni zamu ya Wasomi Twendezetu Kutalii'  limetegua kitendawili cha kwanini  wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Kati ndani ya Mkoa wa Mwanza hawajahamasika kutembelea vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya Kanda ya Ziwa. 



Kongamano hili limekuwa na mafanikio makubwa ambapo jumla ya viongozi wa Serikali za Wanafunzi 100 na wakufunzi 30 kutoka katika jumla ya vyuo vikuu na vya kati 27 wameshiriki.


 Aidha mikakati mbalimbali ya kuhamasisha utalii wa ndani ya Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa imewekwa.



*Tumerithishwa Tuwarithishe*

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI