MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa mkoa utahakikisha unaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili kuondoa changamoto kwenye viwanda.
Kunenge aliyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho na viwanda vingine vya uzalishaji mitungi ya gesi, matenki na mabomba ya maji, kiwanda cha chuma chuma, kiwanda cha uzalishaji jipsam na boti ambavyo vyote viko chini ya kampuni ya Lake Group, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea viwanda mkoani humo ili kujua mafanikio na changamoto zinazowakabili wawekezaji kwenye viwanda.
Kunenge alisema kuwa umeme bado ni changamoto kwani umekuwa ukikatika mara kwa mara lakini mkoa utahakikisha changamoto hiyo inaondoka ili wawekezaji wasipate usumbufu wakati wa uzalishaji.
"Niliwaelekeza watu wa Tanesco kupitia viwanda vyote ndani ya mkoa ili kujua mahitaji yao ya umeme hasa wale wenye matumizi makubwa ili wapewe kipaumbele kwa kuwa na umeme wao na changamoto ya hapa itapatiwa ufumbuzi ili kazi zifanyike kwa ufanisi,"alisema Kunenge.
Akimkaribisha mkuu wa mkoa ofisa mwajiri na rasilimali watu wa kiwanda hicho cha Aluminum Hussein Ally alisema kuwa kwa mwezi wanazalisha matenki 15 na wametoa ajira kwa watu zaidi ya 90.
Naye ofisa mwajiri wa Lake maeneo ya Visiga na Madafu Fadhil Msemwa alisema kuwa wanafurahi kutembelewa viongozi wa ngazi za juu kujua changamoto zao kwani inawapa moyo kuwa wanajaliwa ambapo viwanda hivyo vimetoa ajira rasmi za watu 400 wakiwemo wanaotoka maeneo ya mkoa wa Pwani na maeneo jirani ya mkoa huo.
0 Comments