Header Ads Widget

RC ANDENGENYE:WADAU WA MAENDELEO WANAMCHANGO MKUBWA KUHAMASISHA WAMAMA WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA KWENYE VITUO VYA AFYA

 


Na Editha Karlo,MDTV Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa ushiriki wa wadau wa maendeleo katika kuboresha miundo mbinu ya afya na vifaa tiba kumeweza kuongeza idadi ya mama wajawazito kutumia vituo rasmi wakati wa kujifungua.


Akizundua mpango wa ujenzi wa Chumba cha upasuaji katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya Kasulu inayojengwa kwa ufadhili wa shirika la Medical Team international Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mchango wa wadau wa maendeleo katika sekta ya afya umeleta mabadiliko makubwa mkoani humo.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kwa sasa idadi ya mama wajawazito wanaojifungua kwenye vituo rasmi mkoani humo imeongezeka na kufiikia asilimia 97 hivi sasa kutoka asilimia 91 mwaka 2018 ambapo kwa miaka mitano iliyopita jumla ya mama wajawazito 4237 walijifungua kwenye vituo vinavyosaidiwa na Medical Team International ambapo hakuna kifo cha mama mjamzito wala mtoto kilichotokea wakati wakujifungua.


Akitoa taarifa kuhusu  ujenzi wa chumba hicho cha upasuaji Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Medical Team Internatioanl, Dk.George Mwita alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 202 kinatarajia kutumiwa na shirika hilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa chumba hicho ikiwa ni kutimiza mpango wa kuboresha huduma za afya karibu na wananchi sambamba na kupunguza vifo kutokana na kutopatikana kwa huduma hizo kwa haraka.


Dk.Mwita alisema kuwa  kwa kipindi ambacho Medical Team International imeanza shughuli zake nchini imetumia jumla ya shilingi bilioni 2.4 ambapo kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 1.7 kimetumiwa mkoani Kigoma pekee ikiwa ni pamoja na kusaidia huduma za afya kwa wakimbizi, wananchi kuzunguka maeneo ya kambi na vituo vya utoaji huduma ikiwemo hospitali ya mkoa na wilaya.


Alisema kuwa miongoni mwa uboreshaji wa utoaji huduma ambao taasisi hiyo imefanya ni pamoja na ununuzi wa vifaa kwa ajili ya chumba cha upasuaji hospitali ya mkoa Kigoma Maweni kiasi cha shilingi milioni 131, kusaidia huduma za rufaa kwa wakimbizi na wananchi wa mkoa Kigoma katika hospitali ya rufaa Bugando ambapo kiasi cha shilingi milioni 637.4 zilitumika.


Awali Mganga Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Dk.Bernad Rwebangira alisema kuwa ujenzi wa chumba hicho cha upasuaji utatumia jumla ya shilingi milioni 236.4 ambapo kati ya hizo shilingi milioni 202 zitatolewana Medical Team International na kiasi kinachobaki kitatolewa na halmashauri hiyo.


Dk.Rwebangira alisema kuwa jengo hilo litakapokamilika na kuanza kazi litakuwa na uwezo wa kutoa huduma za upasuaji kwa jumla ya watu 575,191 ikiwemo huduma za upasuaji kwa mama wajawazito wakati wa kujifungua.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI