Header Ads Widget

MTAKA AAGIZA KLABU ZA WATOTO KUAZISHWA SHULENI ILI WAWEZE KUJADILI MASOMO YAO





Na Hamida Ramadhani Dodoma 



MKUU wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amemwagiza Afisa Elimu mkoani Dodoma kuwaandikia barua wakuu wa shule za sekondari za mkoa huo kuhakikisha wanaanzisha klabu za watoto ambazo zitawawezesha kujadili mambo mbalimbali katika Masomo.


Mtaka ameyasema hayo jijini hapa alipotembelea shule ya sekondari ya Nzuguni kuangalia uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2022 huku akisema,kutokana na vyuo vilivyopo katika mkoa wa Dodoma hakuna sababu ya wakuu wa shule kulalamikia upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.


Akitolea mfano wa klabu chache ikiwemo ya kupambana na Rushwa,klabu ya Mazingira pamoja na klabu za masomo mbalimbali huwawezesha watoto kukaa pamoja na kujifunza masuala ya masomo na mambo mengine yakiwem kukataa rushwa .


Aidha Mtaka ameutaka uongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na wakuu wa shule za sekondari kuwa wabunifu na kutumia fursa ya vyuo vikuu vilivyopo mkoani humo kupata walimu wa masomo ya sayansi badala ya kulalamikia upoungufu wa walimu hao kila siku.


“Naomba tutumie ubunifu na fursa kwa watoto walio katika madarasa ya mtihani wafundishwe ipasavyo badala ya kulalamikia upungufu wa walimu wa sayansi ,”amesema.


Na kuongeza kuwa "hatuwezi kusema tuna upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi wakati tuna vyuo hapa mkoani kwetu na uwezo wa kupata wa walimu ambao wamefikia muda wa kufanya mazoezi kwa vitendo ,kwa hiyo hili siyo jambo la kusema tuna changamoto,” Mtaka


Vile vile amewataka walimu wajikite katika kusaidia wanafunzi wa madarasa ya mtihani wa Taifa wajitambue na kuanza maandalizi ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne na cha pili ambayo hufanyika kuanzia mwezi Oktoba kila mwaka.


Katika hatua nyingine Mtaka amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa za mapambano ya UVIKO 19 ambazo zimesaidia ujenzi wa madarasa mapya ambapo katika shule Nzuguni sekondari imepata madarasa 10 na hivyo wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kupata nafasi tofauti na miaka mingine ambayo wanafunzi wamekuwa wakisajiliwa kwa awamu.


Kutokana na ujenzi huo Mtaka ameagiza wanafunzi wa kidato cha kwanza wapewe kipaumbele kutumia madarasa hayo mapya.


Awali Mkuu wa shule ya Sekondari ya Nzuguni Rogers Justinian amesema wanafunzi 583 walipaswa kuripoti na kwamba walioripoti Januari 17 mwaka huu ambapo ndio shule zimefunguliwa ni wanafunzi 401 huku wakiwa hawajaripoti ni 182.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI