Header Ads Widget

M/KITI WA ACT WAZALENDO MKOA WA RUVUMA AISHAURI SERIKALI KUWEKA RUZUKU KWENYE PEMBEJEO .

 



 


MWENYEKITI wa Chama Cha ACT Wazalendo Mkoani Ruvuma Mshamu Ngabuja ameishauri Serikali iangalie namna bora ya kuweka luzuku kwenye Pembejeo (Mbolea)ili kuwasaidia wakulima waweze kununua kwa bei ya chini na hatimaye kumudu shughuli za kilimo............NA AMON MTEGA, _SONGEA.




 Akizungumza na vyombo habari mkoani humo mwenyekiti huyo amesema kuwa kumekuwepo na mfumko wa bei ya vitu ikiwemo suala la pembejeo jambo ambalo linawafanya baadhi ya wakulima hasa wa mikoa ya kilimo kama mkoa wa Ruvuma kushindwa kumudu bei hizo.



 Ngabuja amesema kuwa kama Serikali itaweka luzuku kwenye pembejeo hizo itawasaidia wakulima kununua bei ya chini tofauti na sasa ambapo mfuko mmoja wa mbolea wa kilo 50 unauzwa kuanzia shilingi Themanini na tano kwenda juu   (Sh.85,000=)kulingana na aina ya mbolea jambo ambalo amedai kuwa wengi wao wanashindwa kuzimudu bei hizo .



 Amesema kuwa licha yakuwepo kwa changamoto za hali  ya hewa katika msimu wa mwaka huu  lakini wakulima wengi hasa wa mkoa wa Ruvuma wamelima mashamba yao kwa mvua hizi zinazoendelea kunyesha huku  changamoto kubwa ni suala zima la Pembejeo kuwa bei kubwa.



  Kwa upande wake katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Ruvuma Richard Tawe amesema kuwa ili mkulima aweze kujikwamua kupitia kilimo ni lazima kumsaidia kwenye suala zima la Pembejeo ili mwisho wa siku chakula kiweze kupatikana kwa wingi.



Hata hivyo ameelezea mpango kazi wa chama chao kuwa sasa kinajipanga kwenda kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Taifa.


                 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI