Header Ads Widget

MKAKATI WA KITAIFA WA ELIMU JUMUISHI WA MIAKA MITANO WAZINDULIWA

 


Hamida Ramadhan Dodoma


SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imezindua mkakati wa Kitaifa  wa Elimu jumuishi wa miaka mitano [2021/22-2025/26]lengo likiwa ni kutoa Elimu jumuishi ambayo itakuwa na mfumo ambao unatoa fursa kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum kuanzia ngazi ya awali hadi Chuo.


Akizungumza katika uzinduzi wa Mkakati huo leo Jijini Dodoma Kwaniaba ya Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda,Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka  amesema Mpango wa Serikali ni kuhakikisha  kila Mtanzania anapata elimu bora bila kujali hali aliyo nayo 


" Serikali ipo katika mpango wa kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bira bika kujali mtoto huyo  yupo katika changamoto gani," amesema


Katika hatua nyingine Profesa Sadoyeka ametoa wito kwa wadau wote wa elimu Nchini  kuwa wanafikisha taarifa sahihi juu ya umuhimu wa elimu Jumuishi hasa kwa makundi ya watu wenye mahitaji maalum ili wawwze kupata Elimu.


Kwa Upande wake Kmishna wa Elimu Tanzania  Dkt.Lyabwene Mtahabwa amesema kila mtu ana haki ya kupata elimu bora na kitendo Cha  kumnyima mtu elimu bora ni kumwandaa kuwa mtumwa katika karne hii ya 21.


Awali Mkurugenzi wa Elimu Maalum wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia,Magreth Matonya ameeleza kuwa kupitia Mkakati huo watakuwa wakifanya tathmini mara kwa mara.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI