Header Ads Widget

DC KILOSA AMALIZA MGOGORO ULIODUMU MIAKA 8

 

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga  amefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya Mwekezaji mwakilishi  aliyefahamika kwa jina la Fransica Mtitu na wananchi wa Kijiji cha Mbingiri uliodumu kwa zaidi ya miaka nane.


DC Mwanga amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo na malalamiko kutoka kwa wananachi wa kijiji hicho kukosa maeneo ya shughuli za Kilimo 


 Mwanga anasema baada ya kupata  malalamiko hayo amelazimika kufanya mkutano wa hadhara kati ya wananchi na mwekezaji "Kilosa Mbigiri Farm"ambapo  mwakilishi wa familia ya  Mwekezaji  Gervas Mtitu ameridhia kuachia wananchi  hekari 131 na yeye kubaki na hekari 193.



 " Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan haipo tayari kuona waanchi wake wanapata tabu na  ardhi yao ni vyema wakakabidhiwa ili wajiongezee kipato haswa kilimo cha miwa" Amesema DC Mwanga


Aidha amewataka wananchi kuacha tabia ya kuwauzia maeneo watu wageni na kwamba watumie katika shughuli za Kilimo huku akitoa onyo kwa viongozi wa vijiji kugawa bila upendeleo ni muhimu kipaombele  kiwe ni  vijana na wanawake


Katika hatua nyingine DC Mwanga  amewashkuru sana wananchi wake , kamishna wa ardhi na mwekezaji kwa  kumaliza mgogoro  kwa njia ya amani kwani Jambo la kujivunia .


Kwa uapande wa mwenyekiti wa Kijiji Cha Mbingiri Metodi Peter akizungumza kwaniaba ya wananchi wenzake amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaj Majid Mwanga na viongozi wote kwa ujumla kwa kuwasaidia kumaliza mgogoro huo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS